Kwa nini mawazo ya nyota wengi wa Soka duniani yanafuatilia uchaguzi mkuu wa DR Congo?

Christian Kabasele Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Christian Kabasele anatokea maeneo hayo yaliyo na utajiri mkubwa wa madini yanayotumika kuunda simu za mkononi

Huku mechi kubwa zikichezwa msimu huu wa sherehe, wachezaji nyota kutoka DRC wanafuatalia kwa ukaribu mno kile kinachoendelea nchini mwao.

Raia wa taifa hilo kubwa la Jamhuri ya Demokrasia ya Congo- DRC, wanapiga kura kumtafuta mrithi wa Rais mwenye umri wa miaka 47 Joseph Kabila Kabange siku mbili kabla ya sherehe za krismasi.

Kwa miongo sita tang uhuru wa nchi hiyo, taifa hilo halijawahi kushuhudia upeanaji wa mamlaka kwa njia ya amani, na miaka 20 iliyopita, taifa hilo lilishuhudia vita vibaya mno vilivyopewa jina Africa's World War yaani Vita Vikuu vya Dunia vya Afrika, vilipiganwa katika ardhi ya Congo.

Utovu wa usalama na makundi ya waasi, yangali yakitekeleza uhasama katika maeneo mengi ya nchi hiyo.

''Nimejawa na huzuni kubwa sana, sio tu kwa sababu ya vita, lakini hali nzima ilivyo kwa sasa nchini Congo. Ni huzuni kubwa kuwa na taifa kubwa tajiri lakini raia wake ni masikini kupindukia. sio jambo la kawaida," anasema Christian Kabasele, mlinzi wa timu ya Watford, iliyomo katika ligi kuu ya Premia nchini Uingereza.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Benik Afobe wa Stoke City

Mchezaji huyo wa kandanda alizaliwa Lubumbashi, mji mkuu wa eneo hilo, ambalo lina utajiri mkubwa wa madini ambayo hutumika na kampuni nyingi duniani kutengeneza simu za rununu na bateri ya magari ya kielektroniki.

"Pesa hazisambazwi vyema- ni wanasiasa tu wakuu katika jimbo hilo au vigogo wengine mashuhuri, ndio hujigawanyia pesa hizo. Kinachoniuma zaidi ni sio watu wengi duniani huzungumzia hilo," aliongeza.

"Kuna tatizo katika taifa hili, lakini hakuna anayejali kabisa."

Mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 27- anasema kwamba hajawahi kurudi nyumbani kwao tangu alipoondoka huko akiwa mchanga.

"Nilikuwa na umri wa miezi michache tu, na siwezi kwa yakini kukumbuka kilichotokea. Wazazi wangu waliona kuwa njia bora na muafaka kwangu mimi na kakangu ni kuhamia Ubelgiji."

Ni miongoni mwa idadi kubwa zaidi ya raia wa Congo wanaoishi nje ya nchi, wakiwemo wachezaji mahiri wa soka, ambao walikimbia taifa hilo na kelekea Ulaya kutokana na kudorora kwa uchumi.

Wana matumaini makubwa kuwa uchaguzi mkuu ambao umepangiwa kufanyika siku ya Jumapili, utaleta serikali thabiti na kuwepo na amani ya kudumu.

'Swala Gumu'

Baadhi ya nyota wa soka waliozaliwa barani Ulaya, bado wanajiona kama Wakongomani, akiwemo Benik Afobe, anayeisakatia kabumbu timu ya Stoke City ya England.

"Tangu nilipozaliwa wazazi wangu walinifunza Kilingala, lugha ya Ba-Kongo. Nala chakula cha Kikongomani. Daima nimejihisi kama Mkongomani ndani ya moyo wangu na kwenye damu yangu," anasema Afobe, ambaye pia anaichezea timu ya DR Congo international.

Nahodha wa timu ya soka ya taifa la Ubelgiji pamoja na ile ya Manchester City, Vincent Kompany, ambaye pia alizaliwa ughaibuni, anakiri kuwa asili yake ni Congo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Vincent Kompany wa Manchester City

"Nimekuwa nchini Kongo mara nyingi, hasa Kinshasa na Bukavu. Ni taifa langu, limo moyoni na kila nifanyalo.

"Chochote nifanyacho huwa kiasi kwa Congo na kiasi kwa Ubelgiji.

"Nataka taifa hili lisonge mbele," anasema Kompany.

Ninapoulizwa kuhusiana na hali ya kisiasa ilivyo nchini, mahali ambapo kuna zaidi ya walinda amani 20,000 wa Umoja wa mataifa, na ambao wametumwa huko kwa zaidi ya karne mbili, "ni swala kubwa na ngumu mno."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Lomana Lua-Lua mchezaji wa zamani wa Portsmouth na Newcastle

"Tunachosema hapa ni kwamba, hatma ya baadaye ya taifa lolote ni watoto wake.

"Hata hivyo, lolote tufanyalo kuwaunga mkono ndivyo bila shaka taifa letu litakapoimarika siku za usoni, na bila shaka ni jambo muhimu zaidi kwa bara la Afrika kulinda vijaji vijavyo, kwa kuwekeza kwa watoto."

'Tunataka amani'

Kwa Lomana LuaLua, anayesakatia ngozi timu za Portsmouth na Newcastle kwenye michuano ya ligi kuu ya Premia nchini Uingereza, wakati wa kilele cha uchezaji wake, amesema suluhu ndlo jambo la muhimu kwa sasa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arthur Masuaku wa West Ham United

Mada zinazohusiana