Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 20.12.2018: Pochettino, Pogba, Alderweireld, Solskjaer, Rabiot

Pogba Haki miliki ya picha Getty Images

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino ndio mkufunzi pekee anayetajwa na vyanzo ndani ya Manchester United kuchukua nafasi ya Jose Mourinho aliyetimuliwa Jumanne. United wanajitayarisha kutoa kitita cha pauni milioni 42 ili kumpata raia huyo wa Argentina. (Telegraph)

Paul Pogba alishangilia kwa nguvu taarifa za kufukuzwa kwa Mourinho zilipotangazwa wakati wachezaji wakiwa mazoezini. Hata hivyo, mkufunzi msaidizi Michael Carrick ilibidi aingilie kati na kumuonya Pogba hakuna mtu mkubwa au muhimu zaidi ya klabu. (Sun)

Uhusiano wa Mourinho na Pogba ulikuwa mbaya kabisa katika wiki za hivi karibuni kiasi cha kocha huyo kumwambia mchezaji mmoja (ambaye hakutajwa jina) akae mbali na Pogba. (ESPN)

United watampatia kocha wao wa muda Ole Gunnar Solskjaer kitita cha pauni milioni 50 ili kufanya usajili mwezi ujao. Kiungo wa Juventus na Brazil Douglas na beki wa kati wa Tottenham Toby Alderweireld ndio wanaowindwa zaidi na Mashetani Wekundu. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kocha wa muda wa Man United Ole Gunnar Solskjaer kupatiwa pani milioni 50 kufanya usajili mwezi ujao.

United wanaangazia kurefusha mikataba ya nyota wao wakubwa baada ya Mourinho kuondoka, klabu hiyo inaamini mazungumzo ya kurefusha mikataba yalikuwa yanasuasua kutokana na nyota hao kutokuwa na maelewano mazuri na kocha huyo. (Mirror)

Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane anaangalia uwezekano wa kuchukua nafasi ya Mourinho kama kucha wa Manchester United. (AS)

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anapanga kumsajili kiungo wa Lyon ya Ufaransa Houssem Aouar, 20, ili awe mrithi wa kiungo nyota wa City Fernandinho. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kylian Mbappe, 20, anataka kuwa kocha pale atakapomaliza kusakata kandanda.

Mshambuliaji wa PSG na Ufaransa Kylian Mbappe, 20, amesema anataka kuwa kocha pale atakapomaliza kusakata kandanda. Hata hivyo, kwa umri alonao ni dhahiri kuwa ndoto hiyo bado ni changa. (Le Parisien)

Klabu ya Inter Milan bado inakusudia kumsajili kiungo wa Arsenal Mesut Ozil, 30, ambaye alikuwa benchi jana usiku wakati klanu yake ikifungwa kwenye nusu fainali ya kombe la Carabao na Tottenham . (Mail)

Mchezaji nayeripotiwa kuwaniwa na vilabu vya Liverpool na Barcelona Adrien Rabiot, 23, ni wazi hatokuwepo katika klabu ya Paris St-Germain msimu ujao,hayo yamesemwa na mama yake ambaye pia ndiye wakala wake bi Veronique. (RTL)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Adrien Rabiot

Barcelona wana jianda kumsajili mwezi ujao beki wa kati wa Juventus na Italia Daniele Rugani, 24. (Sport)

Fulham wapo tayari kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth Lys Mousset, 22, mwezi January. (Sky Sports)

Mada zinazohusiana