Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 21.12.2018: De Jong, Ozil, Mourinho, Nasri, Moses

Jose Mourinho

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester City itawalazimu kupambana na vilabu vya Barcelona na Paris St-Germain ili kupata saini ya mchezaji kiungo nyota anayechipukia Frenkie de Jong, 21. Dejong raia wa Uholanzi anayechezea Ajax anakisiwa kuwa na thamani ya pauni milioni 60. (Mirror)

Real Madrid hawana mpango wa muda mfupi au mrefu wa kumwajiri tena Jose Mourinho, 55, aliyefutwa kazi na Manchester United jumanne wiki hii. (Marca)

Crystal Palace wana imanikuwa watafanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Nigeria na Chelsea Victor Moses, 28, katika dirisha la usajili la mwezi ujao. (London Evening Standard)

Rais wa klabu ya Napoli Aurelio De Laurentiis amesema klabu hiyo haitamuuza mlinzi wake kisiki raia wa Senegal Kalidou Koulibaly, 27, kwenda Manchester United mwezi ujao, lakini wanaweza kukubali dau kwa wakati ujao. (Corriere del Mezzogiorno, via Star)

Arsenal wanataka kumuuza mchezaji wao anayepokea mshahara mkubwa Zaidi Mesut Ozil, 30, ambaye bado ana mkataba wa kuchezea Washika Bunduki hao wa London mpaka mwaka 2021. Hata hivyo inaweza kuwawia ugumu Arsenal kupata mnunuzi. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

West Ham watafanya maamuzi wiki ijayo iwapo wanampatia Samir Nasri, 31, mkataba wa muda mfupi amesema kocha Manuel Manuel Pellegrini has revealed. (London Evening Standard)

Mchezaji wa zamani wa West Ham James Collins, 35, amepoteza mkataba wa pauni 50,000 na klabu ya Aston Villa baada ya kuumia saa moja baada ya kusaini mktataba. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Fred hajakuwa na kiwango bora toka alipojiunga na Mashetani Wekundu

Kiungo raia wa Brazil Fred, 25, atapambania mustakabali wake ndani ya Manchester United baada ya kusalia benchi wakati wa uongozi wa kocha aliyefukuzwa Jose Mourinho. (Telegraph)

Evertonkupitia mkurugenzi wao wa mpira Marcel Brands wamesema hawapo tayari kumnunua mchezaji wa PSV raia wa Mexico Hirving Lozano, 23, kwa pauni milioni 30. (Voetbal International)