Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 22.12.2018: Ozil, Isco, Puel, Zidane, Higuain, Morata, Fabregas

Arsenal midfielder Mesut Ozil

Chanzo cha picha, Getty Images

Kocha wa klabu ya Leicester City Claude Puel huenda akafutwa kazi wakati wowote baada ya kupoteza uungwaji mkono kutoka kwa wachezaji wake. (Daily Mail).

Klabu ya Arsenal ya Uingereza inafikiria kufikia makubaliano ya kubadilishana mchezaji wake raia wa Ujerumani, Mesut Ozil mwenye umri wa miaka 30 na wao kumchukua kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Uhispania Isco mwenye umri wa miaka 26. Washika bunduki wa London wako tayari kupokea ofa kutoka kwa klabu nyingine pia (Independent).

Klabu ya Sheffield Wednesday inaelezwa kujiandaa kumpa mkataba wa mwaka mmoja kocha wa zamani wa klabu ya Aston Villa Steve Bruce ili achukue nafasi ya kocha Jos Luhukay ambaye alifutwa kazi Ijumaa ya wiki iliyopita. Sheffield Wednesday inataka kumpa mkataba wa paundi milioni 2. (The Sun).

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Zidane aliisaidia Real kushinda mechi 104 kupata sare mechi 29, na kujipatia asilimia 69.8% ya ushindi mbali na mataji tisa.

Klabu ya Chelsea ya Uingereza imeripotiwa kuwa inafikiria uwezekano wa kupata saini ya mshambuliaji wa AC Milan na timu ya taifa ya Argentina, Gonzalo Higuain mwenye umri wa miaka 31 kwa kubadilishana na mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata mwenye umri wa miaka 26. (Sky Sports).

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Gonzalo Higuain

Kocha wa klabu ya Chelsea Maurizio Sarri amemuelezea Higuain kama mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani kwa sasa. (ESPN).Kocha Sarri pia anaelezwa kuwa asingependa kumtoa kwa mkopo mwezi ujao kiungo wake raia wa Uingereza Ruben Loftus-Cheek mwenye umri wa miaka 22. (Guardian).

Kocha wa klabu wa Monaco ya Ufaransa Thierry Henry anataka kumsajili kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas ifikapo mwezi Januari. Kiungo huyu wa kimataifa wa Uhispania mwenye umri wa miaka 31 anaelezwa kutokuwa na furaha kutokana na kukosa kucheza mechi nyingi msimu huu. (L'Equipe via Daily Mirror).

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Cesc Fabregas

Kocha wa Fulham Claudio Ranieri anafikiria ifikapo mwezi Januari kupata saini ya beki wa kulia wa Uingereza Danny Simpson, ambaye alicheza chini yake wakati akiwa na timu ya Leicester. Mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 31 mkataba waka unatarajiwa kumalizika wakati wa majira ya kiangazi. (Daily Mail).

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Claudio Ranieri

Kiungo wa Ujerumani na klabu ya Brighton Pascal Gross mwenye umri wa miaka 27, ametupilia mbali uvumi kuwa huenda akasajiliwa na klabu ya Liverpool au Southampton (Argus).

Klabu ya Aston Villa inadai kuridhishwa na tabia ya mchezaji wa zamani wa West Ham na timu ya taifa ya Wales, beki James Collins mwenye umri wa miaka 35 na kuna uwezekano wakamwongeza mkataba wa muda mfupi ikiwa atarejea katika kiwango. (Birmingham Mail).

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Crystal Palace Andros Townsend mwenye umri wa miaka 27, amekuwa akiangalia picha za video za mshambuliaji wa Leicester, Jamie Vardy wakati huu anapojaribu nae kucheza nafasi ya mshambuliaji wa kati. (London Evening Standard)

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha,

Andros Townsend

Klabu ya West Ham itakuwa na mashabiki elfu 60 wakati watakapocheza na timu ya Brighton tarehe 2 ya mwezi January baada ya klabu hiyo kupewa hati mpya ya usalama kuongeza idadi ya mashabiki elfu 3. (Football.London).

Bora kutoka Ijumaa

Manchester City watalazimika kupambana na vilabu vya Barcelona na Paris St-Germain ili kupata saini ya mchezaji kiungo nyota anayechipukia Frenkie de Jong, 21. De Jong raia wa Uholanzi anayechezea Ajax anakisiwa kuwa na thamani ya pauni milioni 60. (Mirror)

Real Madrid hawana mpango wa muda mfupi au mrefu wa kumwajiri tena Jose Mourinho, 55, aliyefutwa kazi na Manchester United Jumanne wiki hii. (Marca)

Chanzo cha picha, Getty Images

Crystal Palace wana imani kuwa watafanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Nigeria na Chelsea Victor Moses, 28, katika dirisha la usajili la mwezi ujao. (London Evening Standard)

Rais wa klabu ya Napoli Aurelio De Laurentiis amesema klabu hiyo haitamuuza mlinzi wake kisiki raia wa Senegal Kalidou Koulibaly, 27, kwenda Manchester United mwezi ujao, lakini wanaweza kukubali dau kwa wakati ujao. (Corriere del Mezzogiorno, via Star)

Arsenal wanataka kumuuza mchezaji wao anayepokea mshahara mkubwa zaidi Mesut Ozil, 30, ambaye bado ana mkataba wa kuchezea Washika Bunduki hao wa London mpaka mwaka 2021. Hata hivyo inaweza kuwawia ugumu Arsenal kupata mnunuzi. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

West Ham watafanya maamuzi wiki ijayo iwapo wanampatia Samir Nasri, 31, mkataba wa muda mfupi amesema kocha Manuel Manuel Pellegrini has revealed. (London Evening Standard)

Mchezaji wa zamani wa West Ham James Collins, 35, amepoteza mkataba wa pauni 50,000 na klabu ya Aston Villa baada ya kuumia saa moja baada ya kusaini mktataba. (Mirror)