Mayweather v Nasukawa: Mayweather asema ataburudisha huku Nasukawa akiapa kumuangusha

Floyd Mayweather and Tenshin Nasukawa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Tenshin Nasukawa (kulia) na Mayweather

Mwanamichezo wa kickboxing raia wa Japan ameapa kumuangusha mwanamasumbwi Floyd Mayweather kwenye pigano lao la raundi tatu kesho Jumatatu nchini Japan.

Bingwa wa zamani Mayweather, 41, ambaye alikuwa amestaafu atapigana na Nasukawa kwenye pigano la raundi tatu huko Saitama.

Nasukawa hushindana kwenye shirikisho linalojulikana kama RIZIN la kickboxing.

"Watu nchini Japan sikiliza, Nitamuangusha Mayweather," alisema Nasukawa 20.

Akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari Mayweather ambaye alimshinda Conor McGregor wa UFC mwezi Agosti mwaka 2017 aliahidi kuwa ataburudisha.

Pigano na Jumatatu litafuata sheria za ndondi na litakuwa la raundi tatu za dakika tatu huku Nasukawa akipigwa marufuku ya kurusha mateke.