Tenshin Nasukawa: 'Nimdharau' Mayweather kumbe si mchache

Nasukuwa aliangushwa mara tatu katika raundi ya kwanza kabla ya pigano hilo kusitishwa Haki miliki ya picha Getty Images

Bondia wa Japna anayeweza kupigana kwa mateke na ngumi Tenshin Nasukawa anasema "alimpuuza " Floyd Mayweather lakini pia alikuwa na wasiwasi kabla ya pigano lao ambapo alishindwa na bingwa huyo wa Marekani siku ya Jumatatu.

Mayweather ambaye ni bingwa mara tano wa zamani , na mwenye umri wa miaka 41, alihitaji sekunde 140 pekee kumpiga Nasukawa mjini Tokyo.

Nasukawa, 20, aliangushwa mara tatu kabla ya pigano hilo kusitishwa akibubujikwa na machozi.

"Nimekuwa nikifurahi tangu kuthibitishwa kwa pigano hilo lakini pia nilikuwa na 'wasiwasi," Nasukawa alisema.

Aliandika katika mtandao wake wa Instagram: "Nimevunjika moyo kwasababu nilidhani nitafanya vyema.

"Lakini nitakabliana na ukweli na nitaendelea kukabiliana na changamoto yoyote. Nilijifunza kwamba sikufanya bidii kupata fursa hii, nami nitatumia kushindwa huku ili kujiboresha mwenyewe na kuendelea mbele mwaka huu."

Mayweather alikuwa na uzito wa kilo zaidi ya 4kg (9lb) dhidi ya mpinzani wake katika piganpo lilokuwa na thamani ya dola milioni tisa.

Mabondia wote wawili hawajashindwa katika mapigano yao na matokeo ya mechi hiyo hayataorodheshwa katika rekodi ya Nasukawa.

Alisema "hana majuto" ya kushiriki katika p;igano hilo.

"wakati nilipopata ombi hilo nilikubali kwa haraka," alisema Nasukawa, ambaye pia anafanya mashindano ya martial arts (MMA).

"Nilidhani hii ilikuwa fursa ya maisha, na ingawa kuna tofauti kubwa katika mafanikio na uzito, nilihisi kuwa si lazima kukimbilia changamoto hii.

"lakini licha ya yote yaliotokea kabla ya pigano hilo niligundua kwamba Mayeweather sio mchezo. Mimi ndio nilimdharau.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii