India: Kijiji 'kichafu' kinataka jina jipya

india
Image caption Harpreet Kaur alimuandikia barua waziri mkuu ili wabadili jina la kijiji chake

Kaskazini mwa nchini India, hivi karibuni vijiji vingi vyenye majina ya kudhalilisha kumekuwa na kampeni ya kuhimiza serikali kubadilisha majina hayo.

"Jina la kijiji changu kinaitwa 'Ganda' maana yake ni chafu au haipendezi," Harpreet Kaur alimuandikia waziri mkuu Narendra Modi mwaka 2016 ili waweze kubadili rasmi jina la eneo hilo.

Aliongeza kuwa jina la kijiji peke yake linaweza kuwadhalilisha hata wakazi wa hapo.

"Hali ni mbaya sana, yani hata ndugu zetu huwa wanatutania mara kwa mara ," mwanamke mmoja ambaye ni miongoni mwa watu wanaofanya shinikizo la kubadili jina.

Mwaka 2017, mamlaka ilibadilisha jina la kijiji hicho na sasa kinaitwa 'Ajit Nagar' kikimaanisha fahari ya kaskazini mwa jimbo la Haryana,India.

Kiongozi wa kijiji Lakwinder Ram, alisema kuwa wamekuwa wakijaribu kwa miaka mingi kuishinikiza serikali kubadili majina bila mafanikio.

Licha ya kuwa hakuna mtu ambaye alikuwa hataki kijiji kibadilishwe jina.

Wanakijiji wanasema jina la Ganda lilikuja baada ya mafuriko kuharibu eneo hilo miongo kadhaa iliyopita.

Na afisa aliyetembelea eneo hilo baada ya janga la mafuriko kutokea ndio alitoa jina hilo, kutokana na uchafu uliokuwa umejaa.

Hivyo tangu siku hiyo jina likabaki kuwa ganda yani pachafu.

Wawakilishi wengine wa vijiji 50 wameikasirikia serikali ya India kwa kubadilisha jina hivi karibuni.

Sababu zao zikiwa kwamba majina mengine yanaonekana kama yana ubaguzi, au ya ajabu na yanaleta aibu kwa wakazi wake.

Barua kutoka vijiji 40 zilikuwa zinakubali mabadiliko hao, Krishan Kumar,afisa wa serikali alisema.

Miongoni mwa vijiji vilivyobadilishwa ni kijiji kinachoitwa Kinnar yaani mtu mwenye jinsia mbili.

Hatua za kubadili jina vijiji sio rahisi nchini humo.

Lazima mtu uanze kwa kuishawishi serikali ambayo ndio ina maamuzi ya mwisho.

Kwa wakazi wa kijiji cha Lula Ahir kilichopo jimbo la Haryana jina lilikuwa linawakebei watu wenye ulemavu na harakati za kubadili jina hilo limepitia mlolongo wa urasimu mwingi.

Waliwahi kuiandikia barua serikalini mwaka 2016 na kuwaeleza jinsi wasivyoridhika na jina la kijiji hicho .

Walisubiri majibu kwa miezi sita na kupata majibu ya kukataliwa kwa sababu jina mbadala walilouwa wamelichagua lilikuwa linatumika eneo lingine.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii