Gonzalo Higuain: Kocha wa AC Milan Gennaro Gattuso anahofia Chelsea itamnyakua

Gonzalo Higuain Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gonzalo Higuain(kulia)

Kocha wa AC Milan Gennaro Gattuso amesema kuwa ingelikuwa uwezo wake hangelimwachilia Gonzalo Higuain, kuondoka licha ya madai kuwa Chelsea wanapanga kumnunua.

Mshambuliaji huyo wa Argentina huenda kahamia Stamford Bridge mwezi huu wa Januari kujiunga na Maurizio Sarri, ambaye alikua meneja wake akiwa Napoli.

Kiungo huyo wa miaka 31 amekuwa akichezea AC Milan kwa mkopo kutoka Juventus.

"Mchezaji akifanya uamuzi inakua vigumu kumshauri abadilishe msimamo," alisema Gattuso kumhusu Higuain.

Higuain amepata ufanisi mkubwa chini ya usimamizi wa Sarri, na pia ufungaji wake wa mabao katika ligi ya ulivunja rekodi katika msimu wa mwaka 2015-16.

Amefunga magoli nane katika michuano yote ya Milan msimu huu, baada ya kuondoka Juventus Cristiano Ronaldo alipojiunga nayo mwezi Julai 2018.

Haki miliki ya picha Getty Images

"Uhusiano wetu umejengeka katika msingi wa kuaminiana- tunaambina wazi yaliyo moyoni.''

Gattuso anasema, "Kwa sasa ni mchezaji wetu kwa hiyo tunamweka karibu nasi kadiri ya uwezo wetu.

"Sijui nini kitafanyika akiondoka. Ningelikua uwezo ningelimfunia kwangu nyumbani asitoke."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea