Barcelona: Kevin-Prince Boateng atimiza ndoto yake ya kuondoka Sassuolo

Kevin-Prince Boateng Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Boateng amefunga mabao manne katika mechi 13 akiichezea Sassuolo msimu huu

Kevin-Prince Boateng amekamilisha ndoto yake ya kuhamia Barcelona kwa mkopo kwa kipindi cha msimu uliosalia.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Tottenham na Portshmouth alipewa nafasi ya kurudi katika ligi ya La Liga kwa sababu Barca ilikuwa inahitaji mshambuliaji atakyechukua nafasi ya Luis Suarez.

Boateng alijiunga na timu ya Sasuolo ambayo ni timu yake ya tisa kwa uhamisho wa bila malipo mwaka uliopita na Barcelona wana uwezo wa kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kwa dau la £7.1m .

''Ndoto yangu imekamilika'' , alisema. ''Ni heshima kubwa kwangu mimi kuwa hapa''.

Baada ya kuondoka katika klabu ya Hertha Berlin 2007, Boateng aliichezea klabu ya Spurs na Pompey kabla ya kupata uhamisho wa kwenda AC Milan 2010, akiwasaidia kushinda taji la Serie A katika msimu wake wa kwanza.

Alipongezwa kwa kuwashinikiza wachezaji wenzake wa Milan kutoka uwanjani wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Pro Patria mnamo mwezi Januari 2013 kwasababu ya ubaguzi wa rangi.

Boateng baadaye aliichezea klabu ya Schalke kabla ya kuifungia magoli 10 klabu ya Las Palmas ya Uhispania 2016-2017 na kuisaidia Eintracht Frankfurt kushinda kombe la Ujerumani msimu uliopita .

Alifunga magoli matano kati ya mechi 15 akiichezea Sassuolo msimu huu akijumlisha magoli 61 kati ya mechi 398.

Ijapokuwa alizaliwa nchini UJerumani , aliichezea Ghana mara 15 huku nduguye beki wa Bayern Munich Jerome Boateng akiichezea Ujerumani na walikutana katika kombe la dunia la mwaka 2010 na 2014.

Barcelona walikuwa wana uhaba wa washambuliaji baada ya viongozi hao wa La Liga kumuuza Paco Alcacer na Munir El Haddadi mwezi huu.

''Haonekani kuhitaji muda mrefu ili kuelewa mazingara yake mapya'' , alisema mkufunzi Ernesto Valverde.

Anawajua wachezaji wenzake na anaweza kuanza kucheza mara moja. Yeye anaweza kucheza safu nyingi, kama mshambuliaji wa katikati ama kucheza nyuma ya mshambuliaji mwengine na hata katikati.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Barcelona wana uwezo wa kumsaini Boateng kwa mkataba wa kudumu kwa dau la £7.1m

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii