Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 25.01.2019: Mata, De Ligt, Otamendi, Berta, Clarke, Suarez

Juan Mata Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mkataba wa Juan Mata unaisha mwisho wa msimu.

Klabu ya Barcelona imefanya mazungumzo na kiungo wa Manchester United Juan Mata. Mata, 30, ambaye ni raia wa Uhispania atamaliza mkataba wake na United mwisho wa msimu huu. (Goal)

Manchester City wanataka kumsajili beki wa kati wa Ajax Mholanzi Matthijs de Ligt, 19. Iwapo usajili huo utafanikiwa inatazamiwa beki raia wa Argentina Nicolas Otamendi, 30, anaweza kujiunga na Barcelona. (Sun)

Manchester United wana nia ya kumuajiri mkurugenzi wa michezo wa Atletico Madrid Andrea Berta, lakini klabu ya Atletico imempa mkataba mnono afisaa huyo raia wa Italia. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsenal imekuwa ikimsaka kiungo Denis Suarez lakini juhudi zao zimegonga mwamba kwa sasa.

Kiungo raia wa Uhispania Denis Suarez, 25, anataka kujiunga na Arsenal kwa mkopo, lakini klabu yake ya Barcelona inataka kumuuza kiungo huyo kwa timu za Sevilla ama Real Betis. (Mirror)

Kipa wa Bournemouth na taifa la Bosnia Asmir Begovic, 31, yupo radhi kujiunga na klabu yoyote nyengine kwenye Ligi ya Premia. (Sun)

Fulham wanataraji kumuuza mshambuiaji wao raia wa Ufaransa Aboubakar Kamara, 23, kwa haraka zaidi baada ya kukuamatwa na polisi kwa kupigana katika uwanja wa mazoezi. (Sun)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Aboubakar Kamara (aliyeshika mpira) ameichezea Fulham mechi 15 msimu huu

Klabu ya Yeni Malatyaspor ya Uturuki wanataka kumsajili Kamara licha ya tukio hilo ambapo alimjeruhi mtu. (Guardian)

Klabu ya Sevilla inataka kumsajili winga raia wa Ufaransa Anthony Martial, 23, kutoka Manchester United mwezi huu iwapapo hataafikiana na timu yake kuhusu mkataba mpya na miamba hiyo ya Old Trafford. (Daily Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Anthony Martial

Baba mlezi wa kiungo wa taifa la Colombia James Rodriguez, 27, ambaye yupo Bayern Munich,anafikiria kurudi na kupambana apate nafasi kwenye klabu yake ya Real Madrid. (Evening Standard)

Beki Carl Jenkinson, 26, ametakiwa kupambana ili apate nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal, japo klabu tatu za Burnley, West Brom na Ipswich zimeonesha nia ya kumsajili. (Mirror)

Mada zinazohusiana