Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 26.01.2019: Rabiot, Austin, Tosun, Zaha, Suarez

Adrien Rabiot Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Adrien Rabiot,

Tottenham hatimae wamejitosa katika soko la uhamisho wa wachezaji kwa kumnunua kiungo wa kati wa Paris St-Germain, Adrien Rabiot, 23 kwa kima cha pauni milioni 20. (Sun)

Mshambuliaji wa Southampton Charlie Austin ataondoka klabu hiyo mwezi huu. Tayari Wolverhampton Wanderers na Aston Villa wameonesha nia ya kutaka kumnunua muingereza huyo wa miaka 29. (Telegraph)

Everton wamekataa ombi la Crystal Palace la kutaka kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Uturuki Cenk Tosun, 27. (Liverpool Echo)

Meneja wa Toffees, Marco Silva amemfahamisha Yannick Bolasie,29, kwamba hakuna matumaini ya yeye kucheza msimu huu.

Palace wanatafakari uwezekano wa kumrudisha Silva ambaye alikuwa winga wao wa zamani. (Guardian)

Meneja wa Crystal Palace Roy Hodgson amepuuzilia mbali ripoti zinazodai kuwa winga wa kimataifa wa Ivory Coast, Wilfried Zaha, 26, anaechezea klabu hiyo huenda akajiunga na Borussia Dortmund. (Goal.com)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wilfried Zaha

Real Betis wako tayari kumsaini Emerson, 20, katika hatua ambayo imedidimiza matumaini ya Liverpool na Arsenal ya kupata huduma za beki huyo raia wa Brazil. (Marca)

Leicester wanapania kumsajili kiungo wa kati wa Monaco Youri Tielemans aliye na umri wa miaka 21 na wako tayari kutumia zaidi ya pauni milioni 20. (90min.com)

Arsenal na West Ham wanang'angania kumsainia kiungo wa kati wa Villarreal Pablo Fornals, 22. (Sport, via Talksport)

Arsenal wana matumaini ya kufikia mkataba wa kumsajili Denis Suarez kutoka Barcelona licha ya mazungumzo kuhusu uhamisho wa kiungo huyo wa kati raia wa Uhispania yamekwama. (Evening Standard)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Denis Suarez,wa kati

Mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner, 22, huenda akaongezewa mara mbili mshahara wake katika klabu hiyo baada ya Liverpool kuonyesha nia ya kutaka kumnunua kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani. (Liverpool Echo)

Ombi la mchezaji mpya wa AC Milan Krzysztof Piatek la kuvaa jezi namba tisa mgongoni limekataliwa na klabu hiyo. Hata hivyo kiungo huyo ameambiwa nausimamizi wa klabu kuonesha umahiri wake uwanjani kabla ya kupewa heshima ya kuvaa jezi hiyo maarufu. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Krzysztof Piatek

Kiungo wa kati wa Zenit St Petersburg, Argentine Leandro Paredes, 24, amekubaliana na masharti anayotakiwa kutimiza ili kumuwezesha kuhamia kuhamia klabu ya Paris St-Germain kwa kima cha pauni milioni 35. (RMC Sport)

West Brom wanapigiwa upatu kumsaini kiungo wa kati wa Newcastle Jacob Murphy, 23, baada ya mchuano wao wa kombe la FA dhidi ya Brighton ambapo walitoka sare bila kufungana mabao. (Telegraph)

Crystal Palace wako tayari kumsajili tena winga Bakary Sako kutoka West Brom.

Nyota huyo wa kimataifa wa Mali mwenye umri wa miaka 30, aliondoka uwanja wa Selhurst Park msimu uliyopita. (Guardian)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bakary Sako

AC Milan bado wana matumaini ya kumsaini winga wa Dalian Yifang, Yannick Carrasco.

Mchezaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid na nyota wa kimataifa wa Ubelgiji ana mpango wa kuhamia klab inayoshiriki ligi ya Serie A club nchini Italia. (Calciomercato, in Italian)

Meneja wa Southampton Ralph Hasenhuttl ana mpango wa kupunguza idadi ya wachezaji katika kikosi chake kabla dirisha la uhamisho wa wachezaji kufungwa. (Daily Echo)

Leeds wanamlenga mshambuliaji wa Wolves Ivan Cavaleiro, 25, kutoka Ureno. (Sun)

Tetesi Bora kutoka Ijumaa

Klabu ya Barcelona imefanya mazungumzo na kiungo wa Manchester United Juan Mata. Mata, 30, ambaye ni raia wa Uhispania atamaliza mkataba wake na United mwisho wa msimu huu. (Goal)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mkataba wa Juan Mata unaisha mwisho wa msimu.

Manchester City wanataka kumsajili beki wa kati wa Ajax Mholanzi Matthijs de Ligt, 19. Iwapo usajili huo utafanikiwa inatazamiwa beki raia wa Argentina Nicolas Otamendi, 30, anaweza kujiunga na Barcelona. (Sun)

Klabu ya Sevilla inataka kumsajili winga raia wa Ufaransa Anthony Martial, 23, kutoka Manchester United mwezi huu iwapapo hataafikiana na timu yake kuhusu mkataba mpya na miamba hiyo ya Old Trafford. (Daily Mail)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii