Pep Guardiola asema kuwa Vincent Kompany hatopata mkataba mpya

MKufunzi wa Manchester City Pep Guardiola na Vincent Kompany Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Vincent Kompany alijiunga na Manchester City kutoka Hamburg mwaka 2008 kwa dau la £10m

Nahodha wa klabu ya Manchester City Vincent Kompany hatopewa kandarasi mpya kulingana na mkufunzi Pep Guardiola.

Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 anayeichezea Ubelgiji inakamilika mwisho wa msimu huu .

Ameichezea klabu hiyo mara 14 msimu huu na sasa anauguza jeraha la misuli.

''Ni mchezaji mzuri lakini ukweli ni kwamba katika kipindi cha miaka mitano iliopita amecheza mechi chache'' , chache sana.

''Kwa hivyo hiyo ndio hali tunayoweza kuweka mezani na klabu itajadiliana na ajenti na kufanya uamuzi mzuri''.

''Hatuna wasiwasi kuhusu uwezo wake-tunamkosa sana iwapo hachezi. Yeye ni muhimu ni nahodha wetu na akiwa uwanjani anatupatia cha ziada ambacho mabeki wachache wa katikati duniani wanaweza kutoa''.

Guardiola 'hakuhusishwa katika majadiliano ya kandarasi

Ripoti wikendi zinasema kuwa City ilitaka kumpatia Kompany mkataba wa miezi kumi na mbili lakini hali yake ya maungo ndio ilizua wasiwasi.

Amecheza mechi tatu pekee tangu mwanzo wa mwezi Novemba huku mechi yake ya mwisho ikiwa ushindi dhidi ya Liverpool mnamo tarehe tatu Januari.

Kompany aliwasili katika klabu ya City mwaka 2008 kutoka klabu ya Hamburg na kutia saini kandarasi ya miaka sita hadi mwaka 2012.

Ameiongoza City kushinda makombe matatu ya ligi kuu ya Uingereza, kombe la FA na lile la ligi mara tatu na atatoa ushuhuda wake mwezi Agosti mwaka huu baada ya kuichezea klabu hiyo kwa miaka 10 huku faida kubwa ikipatikana.

''Sihusiki katika mazungumzo'', Guardiola alisema.

''Sio muhimu kufanya uamuzi, lakini lazima wahisi hususan kwa wachezaji ambao wamekuwa hapa kwa kipindi kirefu na kutusaidia kujenga kile tulicho nacho sasa na watu wapya wanaokuja kwa sasa''.

''Sitaki klabu iseme , ni sawa unaweza kuondoka. Wakati huohuo ni muhimu kujua kwamba kuna wakati ambapo ni mwisho kwa kila mtu. Ndio maana nikasema kuwa sio uamuzi wangu''.

''Katika matukio kama hayo, kama Kompany, kama Sergio Aguero kama David Silva, kama bwana Toure awali, ni uamuzi wao kufanya pamoja na klabu. Ni mchezaji muhimu kwa njia nyingi, heshima na kile alichofanya nje na ndani ya uwanja''.

''Anaweza kuzungumza lugha sita tofauti ama hata saba na anazungumza vyema tunamuhitaji''.

''Watu wanaotuwakilisha ni muhimu. Kile walichowafanyia wachezaji wapya na vizazi vipya, huyu ni mchezaji aliyetusaidia kujenga klabu hii na kile tunachojaribu kujenga zaidi''.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii