Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 30.01.2019: Gueye, Benitez, Jovic, Dju, Pogba

Idrissa Gueye Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Idrissa Gueye, 29, anawaniwa na miamba Arsenal, Manchester City na Paris St-Germain

Arsenal na Manchester City wamejiunga katika mbio za usajili wa kiungo wa Everton na timu ya taifa ya Senegal, Idrissa Gueye, 29. (Sky Sports)

Hata hivyo Everton wanasubiri ofa kutoka klabu ya Paris St-Germain kwa ajili ya Gueye. (Daily Mail)

Southampton wamo mazungumzoni na Olympiakos ili wamsajili beki raia wa Norway Omar Elabdellaoui, 27. (Sun)

Arsenal, West Ham na Newcastle wote wametangaza dau kutaka kumsajili kwa mkopo kiungo wa Monaco Mbelgiji Youri Tielemans 21. (Daily Star)

Kinda wa Benfica Mesaque Dju, 19, anatarajiwa kujiunga na West Ham kama mchezaji huru. (Sky Sports)

Real Madrid wanampango wa kumsajili streka wa Eintracht Frankfurt Luka Jovic, 21 - ambaye yupo kwa mkopo kutoka Benfica - ili awa mrithi wa wa streka raia wa Ufaransa Karim Benzema. (AS)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Florentin Pogba kutimkia ligi ya Marekani

Kaka wa nyota Paul Pogba, Florentin, 28, ianatarajiwa kujiunga na klabu ya Atlanta United inayocheza ligi ya soka ya Marekani MLS inayonolewa na Mholanzi Frank de Boer. (L'Equipe)

Liverpool wanahusishwa na usajili wa kiungo kinda wa klabu ya Trabzonspor Abdulkadir Omur, 19, ambaye anawaniwa na klabu kadhaa barani Ulaya kwa sasa. (iNews)

Arsenal itawapa wasubiri mpaka pale Paris St-Germain watakaposajili kiungo wa kati wa pili kabla ya kufikiria kuuaziwa kiungo raia wa Ufaransa Christopher Nkunku, 21. (Get French Football via Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rafa Benitez ana nia ya kuachana na Newcastle mwishoni mwa msimu

Kocha Rafael Benitez kwa mara ya kwanza ameweka wazi kuwa hana hakika kama ataendelea kuiinoa klabu ya Newcastle United baada ya msimu kumalizika. (Independent)

Newcastle wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili kwa mkopo kiungo Andreas Samaris, 29, kutoka Benfica. (Chronicle)

Mada zinazohusiana