Batshuayi, atua Palace, Burnley yamsajili Crouch, Kagawa ajiunga na Besiktas

Dirisha dogo la Usajili la Mwezi januari limefungwa kwa baadhi ya nchini huku nyota kadhaa wakisajiliwa katika vilabu mbalimbali barani ulaya

Klabu ya Crystal Palace, imeongeza nguvu katika safu yake ushambuliaji kwa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji Michy Batshuayi akitokea Valencia ya nchini hispania lakini mchezaji ni mali ya Chelsea.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambuliaji Michy Batshuayi amerejea tena ligi England akitokea Valencia,

Burnley wamesajili Peter Crouch ambae mkataba wake utadumu mpaka mwisho wa msimu, Mshambuliaji huyo alifikisha miaka 38 jumatano tano iliyopita na anakuwa amechezea jumla ya vilabu sita ya Epl.

Mshambuliaji wa Liverpool Lazar Markovic amejiunga na klabu ya Fulham bure, huku mshambuliaji wa klabu hiyo ya Fulham Aboubakar Kamara akijiunga na waturuki wa Yeni Malatyaspor.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Lazar Markovic amejiunga na Fulham

Newcastle United wamevunja rekodi ya ya usajili kwa kutumia kiasi cha pauni milion 20, kumsajili Miguel Almiron kutoka katika klabu ya Atlanta United.

Wajerumani wa Borussia Dortmund wamemtoa kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu, kiungo wake Shinji Kagawa kwenda kujiunga na watukutu wa Kituruki Besiktas.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Shiji kagawa

Leicester City , wao wamemsajili kwa mkopo kiungo toka Monaco,Youri Tielemans huku Monaco wakimchukua Adrien Silva kutokea kwa vija hao wa viunga vya King Power.

Mada zinazohusiana