Tetesi za soka Ulaya Jumatano 06.02.2019: Hazard, Willian, Koulibaly, Bailly, Aarons

Eden Hazard

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 28,anatarajiwa kuiambia klabu hiyo kwamba anataka kuondoka kuelekea Real Madrid mwisho wa msimu huu.. (Telegraph)

Real Madrid wana matumaini ya kumsaini raia huyo wa Ubelgiji na wako tayari kutumia £100m kukamilisha makubaliano hayo. (Mirror)

Kuondoka kwa Hazard kunaweza kusababisha mikataba ya uhamisho, ikiwemo ile ya kiungo wa kati wa Real Madrid Mateo Kovacic, 24, ambaye uhamisho wake wa, mkopo katika klabu hiyo ya Stamford bridge utafanywa wa kudumu pamoja na ule wa kinda wa Uingereza winger Callum Hudson-Odoi, 18, ambaye anauzwa katika klabu ya Bayern Munich. (Sun).

Image caption Chelsea huenda hivi karibuni pia ikampoteza mshambuliaji Willian 30

Chelsea huenda hivi karibuni pia ikampoteza mshambuliaji Willian 30 kwa sababu wanataka kumuongezea kandarasi ya mwaka mmoja raia huyo wa Brazil wakati kandarasi yake itakapokamilika katika kipindi cha miezi 18 , badala ya makubaliano ya muda mrefu. (Evening Standard).

Lengo la Man United katika dirisha la uhamisho la mwisho wa msimu huu ni beki wa kati huku beki wa Napoli Kalidou Koulibaly , 27 akiwa chaguo la miamba hiyo ya Manchester. (Evening Standard).

Image caption Eric Bailey ,24, ameambiwa na kaimu mkufunzi Ole Gunnar Solskjiaer kwamba anasalia kuwa miongoni mwa mipango yake katika klabu ya Old Trafford. (Sun).

Lakini beki wa kati wa United Eric Bailey ,24, ameambiwa na kaimu mkufunzi Ole Gunnar Solskjiaer kwamba anasalia kuwa miongoni mwa mipango yake katika klabu ya Old Trafford. (Sun).

Tottenham ina mipango ya kuimarisha hamu yao ya kumsajili kinda wa Norwich Max Aarons kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho la mwisho wa msimu huu. (Mirror).

Beki wa Denmark Joachim Andersen, 22, anasema kuwa anaendelea kuichezea klabu hiyo ya Itali licha ya ripoti kwamba Tottenham ina hamu ya kumsajili. (Ekstra Bladet via Football London).

Image caption Kiungo wa kati wa Chelsea Tiemoue Bakayoko,24, ana hamu ya kutaka uhamisho wake wa mkopo katika klabu ya AC Milan kuwa wa kudumu. (Football London).

Kiungo wa kati wa Chelsea Tiemoue Bakayoko,24, ana hamu ya kutaka uhamisho wake wa mkopo katika klabu ya AC Milan kuwa wa kudumu. (Football London).

Ombi la Chelsea la £50m kumnunua kiungo wa kati wa Itali Nicolo Barella, 21, lilikubaliwa na klabu ya Cagliari mwezi Januari , lakini mchezaji huyo alikataa uhamisho huo . (Tutto Mercato Web - in Italian).

Gareth Bale anasema kuwa bado hajawasiliana na mkufunzi wake wa zamani Zinedine Zidane tangu goli lake la ushindi katika fainali ya mechi za vilabu bingwa Ulaya dhidi ya Liverpool. (Four Four Two).

Haki miliki ya picha Getty Images

Newcastle ilijaribu kumsaini winga wa Croatia Marko Pjaca ,23, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Fiorentina , wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (Newcastle Chronicle via Corriere Fiorentino).

Klabu ya ligi ya soka nchini Marekani Atlanta United imemsaini Florentin Pogba, 28, nduguye mkubwa wa kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba. (MLS)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii