Everton 0-2 Manchester City: City yapanda juu ye jedwali baada ya kuishinda Everton

Aymeric Laporte akiifungia Manchester City dhidi ya Everton Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Aymeric Laporte aliiweka mbele Manchester City akifunga goli lake la nne msimu huu.

Pep Guardiola anasema kuwa Manchester City wamegundua kutosalimu amri baada ya kurudi katika kilele cha jedwali la ligi kwa mara ya kwanza tangu tarehe 16 Disemba kufuatia ushindi dhidi ya Everton.

Wiki moja iliopita City ilikuwa pointi tano nyuma ya Liverpool lakini ikachukua fursa hiyo baada ya klabu hiyo chini ya ukufunzi wa Jurgen Klopp kupata sare kadhaa na hivyobasi kupanda juu ya miamba hiyo ya Anfield kupitia wingi wa magoli huku wakiwa wamecheza mechi moja zaidi.

''Siku chache zilizopita tungekuwa pointi saba nyuma. Sasa tuko juu ya jedwali. Huu ndio ushauri mkubwa , funzo ni kwamba usikate tamaa'', alisema Guardiola. ''Hili ni funzo kwa wachezaji wote''.

''Jaribu kuendelea kushinda mechi kwasababu maisha yanaweza kubadilika ghafla bin vuu''.

Aymeric Laporte alikutana na mkwaju wa adhabu wa David Silva na kucheka na wavu kwa kutumia kichwa hatua ilioiweka mbele City kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.

Kwa sasa macho yote yataelekezewa Liverpool ambao wanaweza kupanda katika kilele cha ligi iwapo watapata ushindi dhidi ya Bournemouth siku ya Jumamosi, saa 24 kabla ya City kucheza dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Etihad.

Everton itakuwa katika nafasi ya nane baada ya kupoteza kwa mara ya nne katika mechi tano za ligi ya Uingereza katika uwanja wa Goodison Park , ijapokuwa wanafaa kufurahia mchezo mzuri walioimarika ikilinganishwa na mchezo wao katika wiki za hivi karibuni.

Fursa ya Man City huku jedwali likichukua mwelekeo mpya

Siku saba zilizopita, Manchester City ilikabiliwa na uwezekano wa kuwa nyuma kwa pointi saba ya viongozi Liverpool baada ya kushindwa kwa mara ya nne dhidi ya Newcastle.

Klopp alikosa fursa baada ya kutoka sare na Leicester pamoja na West Ham siku ya Jumatatu kufungua milango kwa City kurudi katika kilele cha jedwali kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya kipindi cha wiki saba.

Timu hiyo ya Guardiola ilionekana kuwa na ari ya kuonyesha umahiri wake katika uwanja wa Goodison Park, ikitengeza fursa tatu za wazi katika dakika 20 za kwanza huku Leroy Sane na Laporte wakikaribia kufunga kabla ya Ilkay kugonga mwamba wa goli.

City baadaye ilionekana kuishiwa na maarifa lakini ikafanikiwa kupata goli la kwanza kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika .

Mkwaju wa adhabu wa David Silva kutoka upande wa kushoto ulifungwa na Laporte.

Image caption Aymeric Laporte alikutana na mkwaju wa adhabu wa David Silva na kucheka na wavu kwa kutumia kichwa hatua ilioiweka mbele City kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.

Aguero na Sterling walikosa nafasi za wazi baada ya kipindi cha kwanza , hata licha ya Everton kushindwa kumjaribu kipa wa Manchester City Ederson.

Ushindi huo uliidhinishwa sekunde chache kabla ya mechi kukamilika baada ya Jesus kufunga kwa kichwa baada ya Jordan Pickford kulipangua shambulio lake.

Matokeo hayo yanaiwekea shinikizo Tottenham katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa huo.

Kikosi cha Mauricio Pochetino kiko nyuma ya viongozi hao wa ligi kwa pointi tano na bado watacheza katika uwanja wa Anfield na Etihad kabla ya kukamilika kwa msimu.

Ushindi huo unamaanisha kwamba City ina uwezo, lakini mabadiliko hayo yanaonyesha kuwa haijaulikani ni nani atakyeweza kuibuka mshindi.

Pep Guardiola: Tunatetea ubingwa na tulikuwa katika hali ambayo tungesalimu amri lakini hilo halikufanyika.Tuna mechi nzuri dhidi ya Liverpool.Hawa wachezaji wameonyesha kuwa na ari na matokeo mazuri katika kipindi cha miaka miwili iliopita. Siwezi kuwakosoa?

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii