Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 07.02.2019: Hazard, Coutinho, Isco, Asensio, Maddison, Varane

Hazard Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Chelsea itaitisha zaidi ya £100m kutoka kwa Real Madrid kumuuza Eden Hazard

Chelsea itaitisha zaidi ya £100m kutoka kwa Real Madrid kumuuza Eden Hazard iwapo klabu hiyo ya Uhispania itawasilisha ombo kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 - msimu huu wa joto. (London Evening Standard)

The Blues inakagua hali ya mchezaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil Philippe Coutinho, mwenye umri wa miaka 26, kama mchezaji anayewezakuichukua nafasi ya Hazard. (Independent)

Real Madrid bado ina matumaini ya kumsajili Hazard kwa chini ya £100m na huenda ikamtumia Isco, mwenye miaka 26, au Marco Asensio, mwenye miaka 23, kama sehemu ya makubaliano hayo. (Mail)

Huenda kulengwa kwa Isco pia kutamshangaza rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu. (Star)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Huenda Marco Asensio, akatumiwa kama sehemu ya makubaliano ya Real kumsajili Hazard

Tottenham wana hamu ya kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Leicester na timu ya England James Maddison, kama mchezaji anayeweza kuichukua nafasi ya Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 26, iwapo mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Denmark ataondoka katika msimu wa joto. (Mirror)

Arsenal imemtambua winga wa Genk, Leandro Trossard, mwenye umri wa miaka 24, kama mchezaji wanayemlenga katika msimu wa joto. (Football.London)

Huenda Manchester United ikamlenga mlinzi wa Real Madrid Raphael Varane, mwenye umri wa miaka 25, kama mchezaji mkuu wanayemwinda katika dirisha la msimu wa joto. (Manchester Evening News)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United Andreas Pereira, amefanya mazungumzo na Santos kuhusu uhamisho mwezi uliopita lakini amefichua kwamba 'kwa bahati mbaya haikuwezekana'. (Star)

Mchezaji chipukizi wa Fulham Ryan Sessegnon bado anasubiriwa kukubali mkataba mpya huko Craven Cottage, akiwa ameanza majadiliano mwaka jana. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 ana chini ya mwaka mmoja na nusu katika mkataba wake wa sasa. (London Evening Standard)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ryan Sessegnon (kushoto)

Mustakabali wa Asmir Begovic katika timu ya Bournemouth unatiliwa shaka baada ya kipa huyo mwenye umri wa miaka 31 kuzozana na meneja Eddie Howe. (Mirror)

Manchester United na Manchester City zimehusishwa na mchezaji wa kiungo cha mbele wa Fiorentina Federico Chiesa, mwenye umri wa miaka 21, ambaye pia amezivutia timu za Inter na Juventus, pamoja na Bayern Munich na Real Madrid. (Calciomercato)

Aliyekuwa mmiliki wa Leeds Massimo Cellino, ambaye sasa anaimiliki Brescia, huenda akaitisha kitita kikubwa cha fedha kwa mchezaji wa kiungo cha kati mwenye miaka 18 Sandro Tonali - mchezaji anayelengwa na Liverpool na Chelsea - iwapo klabu hiyo ya Italia itapandishwa katika ligi ya Italia, Serie A msimu huu. (Inside Futbol)

Jurgen Klopp ataitisha usajili wa wachezaji wa kiungo cha ulinzi kwa timu ya Liverpool msimu wa joto. (Sun)

Kaimu Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anapanga safari ya mafunzo katika msimu wa joto, katika kuelekea mpambano wa mwisho wa mwezi wa ligi na wapinzani Liverpool. (Mail)

Walinzi wa Rangers James Tavernier, mwenye umri wa miaka 27, anakiri aliguswa kwa hatua ya Southampton kuonyesha hamu ya kutaka kumsajili wakati wa dirisha la uhamisho mwezi uliopita. (Daily Echo)

Mlinzi wa Aston Villa Tommy Elphick, mwenye umri wa miaka 31, anasisitiza mikataba inayomalizika muda ya wachezaji kadhaa katika klabu hiyo haitoathiri shabaha ya klabu hiyo katika kuinuka kwenye daraja msimu huu. (Express and Star)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii