Tetesi za soka Ulaya Jumapili 10.02.2019: De Gea, Gbamin, Rabiot, Sessegnon, Richarlison, Bielsa, Costa

Kipa wa man United david Degea Haki miliki ya picha Getty Images

Kipa wa Manchester United David de Gea, 28, anasisitiza kulipwa mashahara wa £350,000 kwa wiki ambazo zitamfanya kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi nyuma ya Alexis Sanchez anayelipwa £400,000 kwa wiki . (Mirror)

Tottenham inahofia kwamba mchezaji wanayemlenga kumsajili Adrien Rabiot, 23, kutoka Paris St-Germain huenda akanunuliwa na Liverpool au Barcelona.(Star)

Manchester United ina mpango wa kumsajili beki wa kushoto wa Fulham Ryan Sessegnon 18 kwa dau la paundi milioni 50 (Express)

Everton huenda ikamchukua mkufunzi wa Leeds Marcelo Bielsa iwapo watamfuta kazi mkufunzi Marco Silva. (Mirror)

Chelsea inamfuatilia mshambuliaji wa Everton Richarlison, 21, ambaye pia ananyatiwa na klabu za AC Milan, Paris St-Germain na Atletico Madrid. (Star)

Barcelona inafikiria kuimarisha safu yao ya ulinzi ya kushoto na sasa wanamlenga beki wa Lyon Ferland Mendy, 23, Filipe Luis, 33, wa Atletico Madrid na kinda anayelengwa na Real Betis Junior Firpo, 22,. (Mundo Deportivo)

Manchester United wamewasiliana na wawakilishi wa Tanguy Ndombele kuhusu uhamisho wa kiungo huyo wa kati wa Lyon . (Le 10 Sport)

Haki miliki ya picha Getty Images

Uamuzi wa Beki wa Ajax Matthijs De Ligt wa kujiunga na ajenti maarufu Mino Raiola unaweza kuharibu uhamisho wake katika ligi ya Uingereza ,huku ikiaminika nchini Uholanzi kwamba klabu za Uingereza hazipendelei kufanya kazi na ajenti huyo.. Manchester City, Manchester United, Liverpool, Arsenal, Chelsea na Tottenham zote zinamlenga kinda huyo mwenye umri wa miaka 19. (Mirror)

Winga wa Juventus winger Douglas Costa, 28, ametoa ishara kuhusu hatma yake ya siku zijazo alipopenda ujumbe wa twitter unaomuhusisha na uhamisho wa Manchester United. (Sun)

Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Borussia Monchengladbach Max Eberl anatumai kwamba klabu hiyo itaweza kumshawishi Thorgan Hazard ambaye amehusishwaa na uhamisho wa Liverpool, kutia kandarasi mpya. (Inside Futbol)

Haki miliki ya picha Getty Images

Manchester United na Arsenal watatuma maskauti wao katika mechi ya Jumapili ya debi la East Anglian ili kumchunguza beki wa Norwich anayedaiwa kugharimu £10m Ben Godfrey, 21, ambaye amevutia klabu kama vile Lyon na RB Leipzig. (Mirror)

Manchester City imeharakisha usajili wa kipa Gavin Bazunu, unaomfanya kinda huyo mwenye umri wa 16 kuichezea timu yake ya wachezaji wake wasiozidi miaka 18 siku ya Jumamosi-. (Manchester Evening News)

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii