Man Utd 0-2 PSG: Kimpembe na Mbappe waizamisha Man United

Presnel Kimpembe alipofungia PSG bao la kwanza Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Presnel Kimpembe alipofungia PSG bao la kwanza

Manchester United lazima wafanye kazi ya ziada kufufua ndoto yao ya kushinda taji ya kombe la Champions baada ya kufungwa mabao 2- 0 na Paris St-Germain katika uwanja wa Old Trafford.

Mabao ya Presnel Kimpembe na Kylian Mbappe yaliwapatia ushindi mabingwa wa Ufaransa.

Ushindi wa mara 10 wa United katika mechi 11 chini ya meneja wao wa muda Ole Gunnar Solskjaer ulifufua matumaini yao ya kuwa tena mabingwa wa ulaya.

Hata hivyo matumaini hayo yalizimwa na PSG katika uga wa nyumbani kwa zaidi ya bao moja.

Sasa United wanahitaji miujiza watakapokutana tena na miamba hao wa Ufaransa mjini Paris Machi 6 ili wafuzu kuingia robo fainali.

Matumaini ya Solskjaer yalididimizwa na majeruhi ya Jesse Lingard na Anthony Martial katika kipindi cha kwanza lakini PSG waliimarisha mashambulizi yao bila uwepo kwa wachezaji nyota wao Neymar na Edinson Cavani.

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer

Kitumbua cha United kiliingia mchanga zaidi, baada ya Paul Pogba kutupwa nje dakika ya mwisho ya muda wa ziada alipolishwa kadi ya njano mara ya pili katika hatua ambayo itamkosesha mechi ya marudio.

Solskjaer amefanya kazi ya kuwatia motisha wachezaji baada ya Jose Mourinho kufutwa kazi mwezi Disemba - lakini usiku wa Jumanne ya Februari 12 ulikuwa mrefu kwake tangu alipotua Old Trafford.

United hawastahili kulaumiwa kwa kushindwa, kilichojitokeza katika mechi hiyo ni kwamba hawakuwa na ubavu wa kukabiliana na timu ya Thomas Tuchel hasa baada ya ya lango lau kushambuliwa na kupitia utendakazi wa Di Maria na kasi ya Mbappe.

Haki miliki ya picha Getty Images

Matumaini ya Solskjaer kufanya vyema katika mechi ya marudio huenda yangalipo lakini hali ilivyo kwa sasa huenda kipigo hiki kimetia kikomo azma ya Manchester United kushida taji la Champions.

Di Maria awajibu waliomzomea

Di Maria alihamia Manchester United baada ya kununuliwa wakati huo katika uhamisho wa kuvunja rekodi Ungereza wa £59.7m kutoka Real Madrid.

Lakini nyota huyo wa Argentina hakutumiwa vizuri na meneja wa wakati huo wa United Louis van Gaal, hali ambayo ilimfanya kuhamia PSG kwa mkataba wa £44.3m.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Angel di Maria akisherehekea ushindi wa PSG dhidi ya Manchester United uwanjani Old Trafford

Manchester United na mashabiki wao walishuhudia kile ambacho angeliwafanyia laiti angelikuwa mchezaji wao wakati wa mechi yao dhidi ya PSG.

Di Maria alikua kiungo muhimu katika ufungaji wa mabao ya PSG.

Mashabiki wa klabu hiyo walimshangilia kwa kuonesha thamani yake katika mechi hiyo.

Kumbukumbu ya Champions League

  • Ole Gunnar Solskjaer ameshindwa kwa mara ya kwanza kama meneja wa Man Utd katika mechi zote 12 aliyochezwa chini ya uongozi wake, hii ikiwa pia ndio kipigo kikali walichopewa nyumbani katika mashindano yoyote ya Ulaya.
  • Paris Saint-Germain ni timu ya kwanza ya Ufaransa kushinda Manchester United katika uwanja wa Old Trafford katika shindano lolote barani Ulaya kabla ya mechi ya Jumanne usiku).
  • Kwanzia mwanzo wa msimu wa mwaka 2016-17, ni Cristiano Ronaldo pekee aliyefunga mabao mengi zaidi (mabao16) katika mechi za muondoano za Champions league kuliko Kylian Mbappe wa PSG aliyefunga (mabao 7) kufikia sasa.
  • Timu 34 zilizoshindwa mechi ya kwanza ya muondoano katika Champions League hakuna hata moja iliyofungwa bao zaidi ya moja nyumbani iliyofanikiwa kuendelea mbele katika juhudi ya kuwania taji hilo.
  • Solskjaer ni meneja wa pili wa Manchester United kufungwa mechi ya kwanza ya Champions League,baada ya Louis van Gaal (Ferguson, Moyes and Mourinho wote walishinda).
  • Angel Di Maria ameandikisha rekodi ya kuchangia ufungaji mabao katika Champions League kwa mara ya tatu, na ya kwanza tangu mwezi Septemba 2013 (wakati wa mechi ya Real Madrid dhidi ya Galatasaray).
  • Gianluigi Buffon amekuwa mchezaji wa nne kucheza Champions League akiwa na mika 41 (baada ya Marco Ballotta, Mark Schwarzer na Oleksandr Shovkovskiy); Alishiriki mashaindano hayo mra ya kwanza kabla ya wachezaji Marcus Rashford na Kylian Mbappe kuzaliwa.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii