Tottenham,Madrid zashinda michezo yao ya klabu bingwa ulaya

Spurs Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jan Vertonghen wa Tottenham akishangilia goli la pili kwa timu yake

Tottenham Hotspurs, wakiwa katika dimba lao la nyumbani Wembley, wamechomoza na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Borussia Dortmund kutoka nchini Ujerumani.

Mkorea Heung-Min Son ndie aliyeanza kuwapatika Spurs, goli la kuongoza katika dakika ya 47 ya mchezo, beki Jan Vertonghen akaongeza goli la pili katika dakika ya 83.

Mshambuliaji raia wa Hispania Fernando Llorente, alihitimisha kazi kwa goli la tatu katika dakika ya 86.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos akishangilia ushindi baada ya mchezo kumalizika

Nao mabingwa watetezi wa michuano hiyo Real Madrid, wakiwa ugenini nchini Uholanzi katika dimba Johan Cruijff Arena, wametakata kwa ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya wenyeji wao Ajax.

Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema, aliipatia timu yake goli la kuongoza katika dakika ya 60, Ajax walichomoa goli hilo kupitia kwa Hakim Ziyech katika dakika ya 75,

Zikisalia dakika tatu mchezo kumalizika Marco Asensio, alifunga goli la pili na la ushindi kwa Real Madrid.

Michezo mingine ya michuano hiyo itaendelea wiki ijayo tarehe 19, Liverpool watakuwa wenyeji wa Bayern Munich, huku Lyon wakiwalika Fc Barcelona.

Tarehe 20, Atletico Madrid watacheza na Juventus, nao Schalke 04 wakiwapokea Manchester City.

Mada zinazohusiana