Klabu ya Pro Piacenza yalazwa 20-0 katika mechi ya ligi

Ligi ya Serie C Haki miliki ya picha Getty Images

Iwapo unadhania timu yako imekuwa na msururu wa matokeo mabaya wikendi hii basi fikiria kichapo hiki walichopewa Pro Piacenza katika ligi ya Itali.

Klabu hiyo ya ligi ya Serie C iliowekwa katika kundi A ilishindwa magoli 20-0, 'ndio magoli ishirini bila jibu' na wapinzani wao katika ligi hiyo Cuneo siku ya Jumapili jioni.

Walikuwa nyuma kwa magoli 16 kwa bila wakati wa muda wa mapumziko huku mshambuliaji wa Cuneo Hicham Kanis akifunga magoli sita pekee kabla ya mapumziko naye mshambuliaji mwenza Eduardo Defendi akipata magili matano.

Katika safu ya ulinzi ya Pro Piacenza kulikuwa na matatizo yaliosababisha mvua hiyo ya magoli. Wakiwa chini katika ligi hiyo ya tatu ya Itali, klabu hiyo ya kaskazini ina matatizo makubwa ya ufadhili.

Walipokonywa pointi nane mapema katika kampeni yao na wameripotiwa kushindwa kuwalipa wachezaji wao tangu mwezi Agosti hatua iliosababisha kujiuzulu kwa wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza.

Walishindwa kushiriki katika mechi tatu kabla ya kichapo hicho cha siku ya Jumapili na iwapo hawangeshiriki ingesababisha kupigwa marufuku katika ligi hiyo ya Serie C.

Wageni hao walichezesha wachezaji wao wote.

Lakini Pro Piacenza walilazimika kuanza mechi hiyo wakiwa na wachezaji saba pekee wakiwempo vijana sita.

Huku wakikosa mkufunzi, nahodha wao mwenye umri wa miaka 18 Nicola Cirigliano alilazimika kuchukua wadhfa wa ukufunzi.

Walimaliza mechi hiyo wakiwa na mchezaji mwengijne wa ziada baada ya mmoja ya wachezaji hao kufanikiwa kupata nyaraka za utambulisho wake baada ya mechi kuanza.

Cuneo ilikuwa imefunga magoli 18 pekee katika mechi zake 24 kabla ya mechi ya siku ya Jumapili , lakini ikafanikiwa kuongeza idadi yao ya msimu huu katika dakika 90 zisizo za kawaida.

Huku ikikabiliwa na hali ngumu ya kifedha , Pro Piacenza inatarajiwa kukutana na shirikisho la soka nchini Itali ili kuamua hatma yao manmo mwezi Machi 11.

'Hali ya kushangaza'

Gabriele Gravina, rais wa shirikisho la soka nchini Itali alitaja matokeo ya siku ya Jumapili kama 'matusi kwa soka'.

''Katika kisa kama hiki Shirikisho la soka nchini Itali ilikuwa na jukumu la kutilia mkazo sheria zote'', alisema.

''Jukumu letu ni kulinda hamu ya mashabiki , afya, biashara na uaminifu wa ligi hii. Tulichoshuhudia itakuwa aibu ya mwisho''.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii