Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 21.02.2019: Bale, Hazard, Eriksen, Hudson-Odoi, Blanc, Almiron, Thuram

Gareth Bale

Real wanaweza kuitisha dau la £131m ili kumuuza Bale, ambaye anahusishwa na uhamisho wa Manchester United. (TeleMadrid, via Talksport)

Au Real Madrid huenda ikamwachilia mshambuliaji wa Wales Gareth Bale kuondoka mwisho wa msimu huu na watamtumia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kama chambo katika majadiliano ya kumnunua mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard, 28, ama kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27. (Marca)

Manchester United inatarajiwa kumpatia mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 21, mkataba mpya wa miaka sita baada ya mazungumzo kufua dafu. (Daily Mirror)

Paris St-Germain ina mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Chelsea na Uingereza Callum Hudson-Odoi, 18, ambaye pia analengwa na klabu ya Bayern. (Sun)

Mkufunzi wa zamani wa Ufaransa na Paris St-Germain Laurent Blanc atakuwa miongoni mwa warithi wa kocha wa Maurizio Sarri iwapo Chelsea itaamua kumfuta kazi raia huyo wa Itali wiki ijayo.

Kiungo wa kati wa Paraguay Miguel Almiron alikuwa anachunguzwa na Manchester United kabla ya kujiunga na Newcastle, kulingana na ajenti wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Newcastle Chronicle)

Tottenham inatumai kupiga hatua muhimu katika ufunguzi wa uwanja wao mpya unaoweza kubeba takriban watu 62,062 msimu huu huku majaribio yakipendekezwa kufanyika tarehe 16 na 23 Machi. (London Evening Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images

Chelsea na Liverpool inamchunguza kinda wa miaka 17 Khephren Thuram - mtoto wa aliyekuwa mchezaji wa Ufaransa Lilian Thuram. Mchezaji huyo anayeichezea timu ya Ufaransa ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 bado hajatia kandarasi ya kuwa mchezaji wa kulipwa katika klabu ya Monaco. (Daily Mail)

Beki wa Leicester na Croatia Filip Benkovic, 21, amethibitisha lengo lake la kurudi kuichezea timu hiyo msimu ujao baada ya mkopo wa muda mrefu katika klabu ya Celtic. (Leicester Mercury)

Rais wa La Liga Javier Tebas ni miongoni mwa wanaotaka kumrithi Richard Scudamore kama afisa mkuu mtendaji wa ligi ya Premia nchini Uingereza. (Times)

Mshambuliaji wa Reading na Nigeria Sone Aluko, 30, anakamilisha uhamisho wa kutaka kwenda kuichezea klabu ya China ya Beijing Renhe. (Mail)

AC Milan inamtaka mchezaji anayelengwa na klabu ya Celtic Timothy Castagne baada ya kufurahishwa na mchezo wa beki huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 23 akilipokuwa akiichezea Atalanta katika ligi ya Serie A. (Inside Futbol)

Liverpool inatarajiwa kuzuru Marekani ya kaskazini badala ya bara Asia mwisho wa msimu huu . (Liverpool Echo)

TETESI ZA SOKA JUMATANO

Mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri atafutwa kazi iwapo klabu hiyo itashindwa katika fainali ya kombe la Carabao dhidi ya Manchester City siku ya Jumapili. (Mirror)

Chelsea watamfuta kazi Sarri na kuweza kumlipa £5m - ikiwa ndio malipo ya kiwango cha chini zaidi kulipwa mkufunzi chini ya uongozi wa mmiliki Roman Abramovich. (Sun)

Chelsea imewalenga wakufunzi wa klabu ya Derby Frank Lampard na aliyekuwa kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane kuwa warithi wa Sarri. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anamchunguza kiungo wa kati wa West Ham Declan Rice, 20, winga wa safu ya ulinzi upande wa kulia wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka, 21, na beki wa Leicester wa kushoto Ben Chilwell, 22, huku akiwa na mpango wa kuwanunua wachezaji wachanga wa Uingereza mwisho wa msimu huu. (Sun)

Timu ya Ujerumani Bayern Munich imejiunga na vilabu vingi vinavyomchunguza mchezaji wa Palace Wan-Bissaka. (Mail)

Chanzo cha picha, TF-Images

Manchester United wamemtaja winga wa klabu ya Borussia Dortmund Jaden Sancho, 18, kuwa mchezaji wanayemlenga zaidi, lakini wanahisi kwamba watalazimika kufuzu katika michuano ya vilabu bingwa Ulaya msimu ujao ili kuweza kumnasa mchezaji huyo wa Uingereza. (Mirror)

Manchester City wanatarajiwa kumpatia kandarasi mpya beki wa Ufaransa Aymeric Laporte, 24, kandarasi mpya kutokana na mchezo wake mzuri msimu huu. (Times - subscription required

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United bado wana matumaini ya kuafikia mkataba kuhusu kandarasi mpya ya kipa wa Uhispania David de Gea, lakini kuna wasiwasi kwamba ada ya ajenti inapandisha bei yake. (ESPN)

Aliyekuwa mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger alikutana na rais wa Paris St-Germain Nasser al-Khelaifi katika mashindano ya tenisi ya WTA mjini Doha wiki iliopita, huku kukiwa na uvumi kwamba mabingwa hao wa Ufaransa hawafurahii kazi ya nkurugenzi wa michezo Antero Henrique. (L'Equipe)

Arsenal wanamchunguza kipa wa Burnley Nick Pope, 26, huku wakitafuta kipa wa kuchukua mahala pake Petr Cech,36 ambaye atastaafu mwisho wa msimu huu. (Mail)

Mshambuliaji wa PSG Angel di Maria anasema kuwa uhusiano wake na mkufunzi wa zamani wa Manchester United manager Louis van Gaal ulidorora baada ya kuhoji mbinu yake ya kuwa na usimamizi mkali katika uwanja wa Old Trafford. (Manchester Evening News)

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona wametuma maskauti kumchunguza mshambuliaji wa Ivory Coast na Lille Nicolas Pepe, 23, mshambuliaji wa Ureno,19, Rafael Leao. (France Football)

Tottenham wamejiunga na orodha ya vilabu vinavyomchunguza shambuliaji wa Birmingham Che Adams 22. (Birmingham Mail)

Real Madrid wanakaribia kukamilisha mkataba wa kumsajili beki wa Brazil Eder Militao kutoka klabu ya Ureno Porto. (Marca)

TETESI ZA SOKA JUMANNE

Chanzo cha picha, Getty Images

Liverpool huenda ikawasilisha ombi jingine la kinda wa Borussia Dortmund na Uingereza Jadon Sancho baada ya kumkosa alipokuwa katika klabu ya Manchester City. (Mirror)

Wolves wanakaribia kumpatia kiungo wa kati wa Morocco Romain Saiss mkataba mpya, 28. (Telegraph)

Arsenal itajaribu tena kumsaini kiungo wa kati wa Sevilla na Argentina Ever Banega, 30, mwisho wa msimu huu (Mirror)

Stoke itajaribu kumuuza mshambuliaji Saido Berahino muda tu dirisha la uhamisho la mwisho wa msimu huu litakapofunguliwa baada ya mchezaji huyo wa Burundi kukamatwa kwa tuhuma za kunywa pombe na kuendesha gari. (Mail)

Barcelona wanapigiwa upatu kumsaini mshambuliaji wa Benfica Luka Jovic, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Eintracht Frankfurt. Real Madrid, Chelsea na Bayern Munich pia zinamnyatia kungo huyo mwenye umri wa miaka 21 kutoka Serbia (Goal)

Mabingwa wa ligi ya Uhispania wanakamilisha usajili wa beki wa kati wa Brazil Vitao, 19, kutoka Palmeiras. (Marca)

Chanzo cha picha, Getty Images

Juventus wameiuliza Inter Milan kuhusu hatma ya Mauro Icardi lakini hawajaanza mazungumzo na mshambuliaji huyo wa Argentina ,25 ama ajenti wake. (Radio Rai via Four Four Two)

Kiungo wa kati wa Newcastle na Senegal Mo Diame, 31, anakaribia kuandikisha kandarasi mpya katika uwanja wa St James' Park. (Chronicle)

Kiungo wa kati wa Norway Martin Samuelsen, 21, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya VVV Venlo, anatarajiwa kurudi nyumbani kwao na klabu ya FK Haugesund. (Inside Futbol)

Kiungo wa kati wa West Brom na Uingereza Rekeem Harper, 18 anakaribia kutia saini kandarasi mpya (Express and Star)