Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 22.02.2019: Koulibaly, Puel, Benitez, Guendouzi na Rashford

rashford

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona ina hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya England Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 21. (Mundo Deportivo)

Ajenti wa Manchester United anayemlenga Kalidou Koulibaly ametupilia mbali tuhuma kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 mchezaji wa Napoli na timu ya taifa ya Senegal anajiunga na Juventus. (Sky Sports)

Leicester itafikiria kumuajiri meneja Newcastle boss Rafael Benitez atakayeichukua nafasi ya meneja Claude Puel aliyeahirisha mazungumzo ya mkataba na St James' Park kushughulika na changamoto ya kuiondoa timu kwenye nafasi ya kushushwa kwenye daraja. (Daily Mirror)

Puel amefanya mazungumzo na naibu kapteni wa Leicester Kasper Schmeichel baada ya babake kipa huyo kupendekeza kwamba mwanawe anataka kuichezea timu kubwa, na kwamba Puel hana uwezo wa kuwatia moyo wachezaji wake.(Leicester Mercury)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kasper Schmeichel alijuunga na Leicester City mnamo 2011 kutoka Leeds United

Meneja wa Arsenal Unai Emery amepuuzia taarifa kwamba Paris St-Germain inafikiria uhamisho wa thamani ya £60m kwa mchezaji wa Gunners anayeichezea timu ya taifa ya Ufaransa ya wachezaji wa chini ya miaka 21 Matteo Guendouzi (Football.London)

Kipa wa Fulham raia wa Uhispania Sergio Rico anasema anataka kusalia hata baada ya muda wa mwisho kuwadia wa mkataba wake wa mkopo kutoka kwa Sevilla. (Sky Sports)

Barcelona inamsaka winga wa Lille na timu ya taifa ya Ivory Coast Nicolas Pepe, mwenye umri wa miaka 23, ambaye amekuwa akilengwa na Arsenal. (Sport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Kapteni wa timu ya Liverpool ya wachezaji wa chini ya miaka 18 Paul Glatzel, aliyefunga mabao mara 23 kwa timu hiyo ya vijana msimu huu, amesaini mkataba wake wa kwanza wa kazi.(Liverpool Echo)

Stoke inatafakari uwezekano wa kumfuta mchezaji wa kiungo cha mbele raia wa Burundi Saido Berahino huku kukiwepo taarifa za kukosana kutokana na kesi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kuhusu kuendesha gari akiwa amelewa. (Mail)

Mlinzi wa Mallorca raia wa Uhispani Antonio Raillo, mwenye umri wa miaka 27, anasema alikataa 'nafasi nzuri mno' kusajiliwa Nottingham Forest katika dirisha la uhamisho mwezi Januari. (AS, kupitia Nottingham Post)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Je ndio mwisho wa mchezaji raia wa Burundi Saido Berahino huko Stoke?

Hull inatizama mchezaji wa kiungo cha kati wa Motherwell raia wa Uskotchi Jake Hastie, aliye na umri wa miaka 19. (Hull Daily Mail)

Manchester United imewaonya mashabiki wa Liverpool kuhusu "msimamo uliokwama" katika kuwadia mechi baina ya timu hizo mbili uwanjani Old Trafford siku ya Jumapili. (Liverpool Echo)

Wakati huo huo mechi ya kufuzu kwa robo fainali ya Manchester United katika kombe la FA dhidi ya Wolves imetatiza mipango ya kuandaa mchuano wa derby dhidi ya Manchester City katika wiki ya kwanza ya Aprili. (ESPN)

Mkuu wa Tottenham Mauricio Pochettino anatarajia kuipeleka timu yake kwa mazoezi katika msimu wa joto mwezi ujao katika kipindi ambacho watakuwa na wiki tatu bila mpambano wowote. (Football.London)