Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 23.02.2019: Zidane, Rakitic, Holland, Ospina, Rabiot

Zinedine Zidane

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Zinedine Zidane,Kocha wa zamani wa Real Madrid

Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane hatazuiliwa na marufuku ya usajili ya Chelsea kuwa meneja mpya katika uga wa Stamford Bridge.

Huenda akatumia euro milioni £200 wakati wa rufaa ya The Blues. (The Sun)

Chelsea huenda pia wakamchukuwa naibu meneja wa England Steve Holland endapo watamfuta kocha mkuu Maurizio Sarri wiki ijayo. (Daily Telegraph)

Vilabu vingine vinne vya lligi ya primia vinakabiliwa na hatari ya kupigwa marufuku ya usajili kwa kukiuka sheria ya kuwasajili wachezaji wadogo. (Daily Mail)

Chelsea watakabiliwa na ushindani kutoka kwa mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich katika juhudi zao za kumnunua kiungo wa kati wa Barcelona, mcroatia Ivan Rakitic, 30. (The Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ivan Rakitic(kushoto)

Arsenal wamempatia kazi ya mkurugenzi wa kiufundi wa Roma Monchi.

Raia huyo wa Uhispania wa miaka 50 aliwahi kufanya kazi na meneja wa Arsenal Unai Emery akiwa Sevilla ambako alitengeneza jina kwa kuwasajili wachezaji kama vile Dani Alves na Ivan Rakitic.(Mirror)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 23 anayechezea Paris St-Germain, anapigiwa upatu kujiunga na Tottenham au Liverpool, baada ya ajenti kukosa kujiunga na Barcelona. (Sport, via Talksport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Adrien Rabiot

Napoli wanakaribia kumsajili kipa wa Arsenal na Colombia David Ospina, 30. (Calciomercato)

Milan Skriniar wa Inter Milan anakaribia kutia saini mkataba mpya na klabu hiyo.

Beki huyo wa kati raia wa Slovakia anadiwa kulengwa na Manchester United. (Sky Italia via Calciomercato)

Mwenyekiti wa PSG Nasser Al-Khelaifi amesema kuwa klabu hiyo haitalazimishwa kuwauza Neymar, 27, na Kylian Mbappe, 20, kwasababu ya masharti ya Uefa ya usawa wa kifedha. (ESPN)

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Kylian Mbappe(kushoto)

Bayern Munich wanatarajiwa kiumsaini mshambuliaji wa kimatifa wa Ivory Coast Nicolas Pepe,23, anayechezea Lille.

Arsenal, PSG na Barcelona pia wana hamu ya kumsajili nyota huyo ambaye ameifungia klabu yake ya Ufaransa mabao 16 msimu huu. (Le10 Sport in French)

Everton wanatafakari uwezekano wa kumsajili beki wa kulia wa PSG Thomas Meunier, 27.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amecheza katika kikosi cha kwanza cha mechi 13 za PSG msimu huu. (Le10 Sport, via Sun)

Tetesi bora kutoka Ijumaa

Manchester United imewaonya mashabiki wa Liverpool kuhusu "msimamo uliokwama" katika kuwadia mechi baina ya timu hizo mbili uwanjani Old Trafford siku ya Jumapili. (Liverpool Echo)

Barcelona ina hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya England Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 21. (Mundo Deportivo)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Marcus Rashford(kulia)

Ajenti wa Manchester United anayemlenga Kalidou Koulibaly ametupilia mbali tuhuma kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 mchezaji wa Napoli na timu ya taifa ya Senegal anajiunga na Juventus. (Sky Sports)

Barcelona inamsaka winga wa Lille na timu ya taifa ya Ivory Coast Nicolas Pepe, mwenye umri wa miaka 23, ambaye amekuwa akilengwa na Arsenal. (Sport)