Tetesi za soka Ulaya Jumapili 24.02.2019: Wan-Bissaka, Joelinton, Saul, Rakitic, Hart, Rondon, Meunier

Saul Niguez wa Atletico Madrid

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona iko tayari kutoa dau la £95m kwa kiungo wa kati wa Atletico Madrid Saul Niguez, 24, ambaye pia amehusishwa na uhamisho wa Chelsea. (AS)

Arsenal inaongoza katika kumwania beki wa kulia wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka, 21, ambaye anadaiwa kugharimu £40m. (Sun)

Newcastle imeajiandaa kuvunja rekodi yake ya uhamisho na imekubali kumsaini mchezaji wa Brazil Joelinton 22 kwa dau la £51m kutoka Hoffenheim mwisho wa msimu huu. (Sport1, via Star)

Manchester United na Bayern Munich wanamfuatilia kiungo wa kati wa Croatia na Barcelona Ivan Rakitic, 30. (Mundo Deportivo)

Kipa wa Burnley na Uingereza Joe Hart, 31, huenda akahamia katika ligi ya MLS. (Sun)

Mshambualiji Salomon Rondon, 29, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Newcastle kutoka West Brom, amefichua kuwa anafurahia kusalia katika klabu hiyo hata baada ya mwisho wa msimu huu (Newcastle Chronicle)

Everton imeanza mikakati ya kutaka kumsaini beki wa Paris St-Germain Thomas Meunier, 27. (Le10Sport, via Talksport)

Arsenal inataka kumrudsha winga wake wa zamani Marc Overmars kama mkurugenzi wa kiufundi lakini mpango huo unazuiliwa na klabu yake ya sasa club Ajax.(Mirror)

Arsenal itampatia Rob Holding, 23, mkataba mpya baada ya kupata jeraha la muda mrefu mwezi Disemba. (Mirror)

Beki wa Brazil Marcelo yuko tayari kuondoka Real Madrid na Juventus wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Calciomercato)

Muonekano wa Roy Hodgson alipoanza kazi yake ya ukufunzi na muonekano wake wa sasa akiifunza Crystal Palace unampiku Sir Bobby kuwa mkufunzi mzee zaidi katika ligi ya Premia.

Kiungo wa kati wa Barcelona Ivan Rakitic, 30, anasema kuwa anataka kusalia katika klabu hiyo ya Nou Camp baada ya kuulizwa maswali mingi kuhusu kuondoka kwake.. (Marca)

Mkufunzi wa Leicester Claude Puel amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kuunga mkono kikosi chake kichanga baada ya kupoteza mechi yao ya nne nyumbani.. (Leicester Mercury)

Mkurugenzi wa klabu ya Liverpool Billy Hogan anasema fedha zitakuwepo kwa mkufunzi Jurgen Klopp mwisho wa msimu huu. (Liverpool Echo)

Tetesi za soka Ulaya Jumamosi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Zinedine Zidane,Kocha wa zamani wa Real Madrid

Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane hatazuiliwa na marufuku ya usajili ya Chelsea kuwa meneja mpya katika uga wa Stamford Bridge.

Huenda akatumia euro milioni £200 wakati wa rufaa ya The Blues. (The Sun)

Chelsea huenda pia wakamchukuwa naibu meneja wa England Steve Holland endapo watamfuta kocha mkuu Maurizio Sarri wiki ijayo. (Daily Telegraph)

Vilabu vingine vinne vya lligi ya primia vinakabiliwa na hatari ya kupigwa marufuku ya usajili kwa kukiuka sheria ya kuwasajili wachezaji wadogo. (Daily Mail)

Chelsea watakabiliwa na ushindani kutoka kwa mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich katika juhudi zao za kumnunua kiungo wa kati wa Barcelona, mcroatia Ivan Rakitic, 30. (The Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ivan Rakitic(kushoto)

Arsenal wamempatia kazi ya mkurugenzi wa kiufundi wa Roma Monchi.

Raia huyo wa Uhispania wa miaka 50 aliwahi kufanya kazi na meneja wa Arsenal Unai Emery akiwa Sevilla ambako alitengeneza jina kwa kuwasajili wachezaji kama vile Dani Alves na Ivan Rakitic.(Mirror)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 23 anayechezea Paris St-Germain, anapigiwa upatu kujiunga na Tottenham au Liverpool, baada ya ajenti kukosa kujiunga na Barcelona. (Sport, via Talksport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Adrien Rabiot

Napoli wanakaribia kumsajili kipa wa Arsenal na Colombia David Ospina, 30. (Calciomercato)

Milan Skriniar wa Inter Milan anakaribia kutia saini mkataba mpya na klabu hiyo.

Beki huyo wa kati raia wa Slovakia anadiwa kulengwa na Manchester United. (Sky Italia via Calciomercato)

Mwenyekiti wa PSG Nasser Al-Khelaifi amesema kuwa klabu hiyo haitalazimishwa kuwauza Neymar, 27, na Kylian Mbappe, 20, kwasababu ya masharti ya Uefa ya usawa wa kifedha. (ESPN)

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Kylian Mbappe(kushoto)

Bayern Munich wanatarajiwa kiumsaini mshambuliaji wa kimatifa wa Ivory Coast Nicolas Pepe,23, anayechezea Lille.

Arsenal, PSG na Barcelona pia wana hamu ya kumsajili nyota huyo ambaye ameifungia klabu yake ya Ufaransa mabao 16 msimu huu. (Le10 Sport in French)

Everton wanatafakari uwezekano wa kumsajili beki wa kulia wa PSG Thomas Meunier, 27.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amecheza katika kikosi cha kwanza cha mechi 13 za PSG msimu huu. (Le10 Sport, via Sun)