Pep Guardiola: Ushindi wa Manchester United dhidi ya Liverpool utaimarisha ushindani wa EPL

Pep Guardiola

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Pep Guardiola ameshinda makombe 23 kama mkufunzi

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anatumai kwamba Manchester United itailaza Liverpool siku ya Jumapili ili timu yake kupanda juu katika kilele cha jedwali.

City inelanga kulihifadhi kombe la Carabao kwa kuishinda Chelsea katika uwanja wa Wembley baada ya United kucheza dhidi ya Liverpool ambao wako sawa kwa pointi na City katika uwanja wa Old Trafford.

''Ni wazi kwamba itakuwa bora iwapo United itapata ushindi'' , alisema Guradiola.

''Lakini sasa ni mwezi Februari na ni ndoto kuzungumzia kushinda mataji manne''.

City ilikuwa nyuma kwa pointi saba mnamo tarehe 19 mwezi Januari lakini mchezo mzuri wa kikosi cha Guardiola umemfanya kocha huyo kuwa na matumaini zaidi ya kuweza kushinda makombe manne ya ligi kuu nchini Uingereza.

Mbali na kutetea mataji yao ya ligi ya Uingereza pamoja na kombe la Carabao City imefika katika hatua ya robo fainali ya kombe la FA dhidi ya against Swansea na ilichukua uongozi wa 3-2 dhidi ya Schalke nchini Ujerumani katika mkondo wa kwanza wa kombe la vilabu bingwa Ulaya wiki hii.

Guardiola ambaye ametaja makombe hayo matatu kuwa furaha kubwa, alisema kuwa tuko katika fainali na tunapofika fainali itakuwa mechi muhimu zaidi msimu huu.

''Pengine kwa United au Liverpool kombe la ligi sio muhimu kwa sababu wana mataji mengi sana lakini sio kama sisi''.

''Kulihifadhi kombe hilo itakuwa kitu muhimu, kushiriki katika fainali ni vyema''.

''Niulize swali hili kuhusu kushinda mataji manne mnamo mwezi Aprili ama Mei na nitajibu swali lako. Siwezi kukudanganya mwezi Mei''.

"lakini sasa mwezi Februari na haiwezekani kuzungumzia hilo. ni kama kiwiliwili .

''Ni mara ngapi nchini Uingereza ambapo tmu moja imeshinda mataji manne msimu mmoja''.

''Musituwekee shinikizo hiyo . Historia ya Alex Ferguson haukuweza kufanya hivyo ''.

''Liverpool miaka ya 80 walishinda mataji mengi ya kombe la vilabu bingwa lakini haikuweza kufanya hivyo''.