Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 25.02.2019: Rodgers, Neymar, Mbappe, Ivan Rakitic, Wan-Bissaka, Hazard

Neymar, 27, na Kylian Mbappe

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Neymar na Kylian Mbappe

Rais wa Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi amesisitiza kuwa klabu hiyo haitamuuza mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymar, 27, na Kylian Mbappe mwaka huu (Marca)

Manchester United imehusishwa na usajili wa kiungo wakati wa Ureno Bruno Fernandes, 24. (A Bola, via Mail)

Meneja wa zamani wa Everton na Manchester United David Moyes amekiri kuwa anawania nafasi ya umeneja wa Leicester iliyoachwa wazi. (BeINSports, via Liverpool Echo)

Arsenal inaongoza katika kinyang'anyiro cha kumuwania beki wa kulia wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka,21, na iko tayari kufikia bei ya euro milioni 40m iliyoitishwa na klabu yake. (Sun)

Leicester City iko tayari kuilipa Celtic euro milioni sita kumnunua Brendan Rodgers kama meneja wao mpya baada ya kumfuta kazi Claude Puel siku ya Jumapili. (Sun)

Chanzo cha picha, SNS

Maelezo ya picha,

Brendan Rodgers

Meneja wa zamani wa Chelsea na Manchester United Jose Mourinho anaamini kuwa kiungo wa kati wa Ubelgiji Eden Hazard atafanya vyema Real Madrid endapo ataamua kuhamia klabu hiyo ya Uhispania. (London Evening Standard)

Mourinho ana panga kurejea kazini msimu huu. (ESPN)

Chanzo cha picha, Science Photo Library

Maelezo ya picha,

Eden Hazard

Arsenal huenda isimpate Marc Overmars kama mkurugenzi wa kiufundi kwasababu Ajax amekataa kumuachilia na haiko tayari kulipwa ofa yoyote, kwa mujibu wa ripoti. (Sun)

Kipa wa Burnley na Uingereza Joe Hart, 31, huenda akahamia katika ligi ya MLS. (Sun)

Manchester United na Bayern Munich wanamfuatilia kiungo wa kati wa Croatia na Barcelona Ivan Rakitic, 30. (Mundo Deportivo)

Rakitic amesema kuwa kuwa anataka kusalia Nou Camp baada ya kuulizwa maswali mingi kuhusu kuondoka kwake.. (Marca)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ivan Rakitic(kushoto0

Bora kutoka Jumapili

Newcastle inajiandaa kuvunja rekodi yake ya uhamisho na imekubali kumsaini mchezaji wa Brazil Joelinton 22 kwa dau la £51m kutoka Hoffenheim mwisho wa msimu huu. (Sport1, via Star)

Barcelona iko tayari kutoa dau la £95m kwa kiungo wa kati wa Atletico Madrid Saul Niguez, 24, ambaye pia amehusishwa na uhamisho wa Chelsea. (AS)

Chanzo cha picha, Getty Images

Everton imeanza mikakati ya kutaka kumsaini beki wa Paris St-Germain Thomas Meunier, 27. (Le10Sport, via Talksport)