Tuzo za filamu za Sinema SZIFF 2019: Tamasha hilo lilianzishwa ili kuongeza thamani filamu za Tanzania

Watoto wang'ara katika tuzo za filamu za Sinema Zetu International (SZIFF 2019). Kwa picha hivi ndivyo mambo yalivyokua.

Tuzo za mwaka huu zimezua gumzo katika mitandao ya kijamii hasa kuhusu vigezo vilivyotumika kuwapa ushindi waigizaji watoto.
Maelezo ya picha,

Tuzo za mwaka huu zimezua gumzo katika mitandao ya kijamii hasa kuhusu vigezo vilivyotumika kuwapa ushindi waigizaji watoto.

Maelezo ya picha,

Bango linaloonesha baadhi ya wasanii waliyoshirikishwa katika tuzo hizo.

Maelezo ya picha,

Watoto kutoka mkoani iringa waliwabwaga mastaa wakubwa katika tuzo za filamu za Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF 2019) wakiwamo Monalisa, Wema Sepetu, Johari, Gabo na Hemed Suleiman.

Maelezo ya picha,

Masanii na mwanamitindo Hamisa Mobeto akifuatilia matukio katika tuzo hizo.

Maelezo ya picha,

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ruby akiingia ukumbuni kuwatumbuiza watu.

Maelezo ya picha,

Mratibu wa SZIFF, Sofia Mgaza, alisema tamasha hilo walilianzisha kwa ajili ya kuongeza thamani ya filamu za Tanzania

Maelezo ya picha,

Msanii mchekeshaji wa Kenya Davis Hezron Mwabili maarufu kama Mwala akifuatilia matukio katika tuzo hizo.

Maelezo ya picha,

Wageni waalikwa walikuwa Naibu Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson,Waziri wa Habari, Dk Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar miongoni mwa wengine

Maelezo ya picha,

Kilele cha tuzo hizo kilifanyika usiku wa kuamkia jana katika ukumbi wa Mlimani City na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.

Maelezo ya picha,

Mmoja wa wasanii waliyotumbuiza usiku wa tuzo hizo.

Maelezo ya picha,

Baadhi ya wasanii wa filamu nchini Tanzania wakipokea zawadi yao

Maelezo ya picha,

Msanii Ruby akiwatumbuiza wageni waalikwa.

Maelezo ya picha,

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akisoma alikuwa mmoja wa wageni waalikwa.

Maelezo ya picha,

Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji, Elia Mjata, amesema ushindi wa watoto katika tuzo za mwakuu umefungua fursa ya kuzalisha vipaji vipya vyenye umri mdogo.

Maelezo ya picha,

Vipengele vilivyokuwa vikitazamwa zaidi ni vya msanii bora wa kike,msanii bora wa kiume na filamu bora ambavyo vilitegemea kura za watazamaji.