Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 26.02.2019: Sarri, Kepa Arrizabalaga, Leicester, Rodgers, Arsenal, Wan-Bissaka

Kepa Arrizabalaga Haki miliki ya picha Getty Images

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri alimgombeza kipa Kepa Arrizabalaga kwa kupuuza amri yake ya kumtaka kutoka uwanjani wakati wa finali ya kombe la Carabao. (Sun)

Kisa hicho kiliwafanya wachezaji wengi wa Chelsea kumkasirikia kipa huyo wa miaka 24 raia wa Uhispania. (Daily Express)

Leicester City imeongeza juhudi za kumuajiri Brendan Rodgers kutoka Celtic kama meneja wao mpya. (Guardian)

Leicester pia inatathmini uwezekano wa kumuajiri meneja wa muda kuchukua nafasi ya Claude Puel hadi mwisho wa msimu huu. (Leicester Mercury)

Manchester United na Chelsea wanamnyatia nahodha wa AC Milan Alessio Romagnoli.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alessio Romagnoli

Lakini huenda wakakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa mabingwa wa Serie A, Juventus. (Calciomercato, via Manchester Evening News)

Mmiliki wa Leeds United Andrea Radrizzani huenda akalazimika kuuza klabu hiyo endapo itashindwa kupanda ngazi ya kushiriki ligi ya primia. (Daily Mail)

Meneja wa Burnley Sean Dyche, amepuuzilia mbali tetesi kuwa analengwa na Leicester. (Burnley Express)

Arsenal inaongoza katika kinyang'anyiro cha kumuwania beki wa kulia wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka,21, na iko tayari kufikia bei ya euro milioni 40 iliyoitishwa na klabu yake. (Sun). (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Aaron Wan-Bissaka

Nahodha wa zamani wa Manchester United Gary Neville anasema kuwa kutakuwa na ''uasi'' Old Trafford ikiwa klabu hiyo haitamuajiri Ole Gunnar Solksjaer kama meneja wake wa kudumu. (Daily Mirror)

Chelsea inajiandaa kumuuza muingereza Kasey Palmer kwa euro milioni nne, licha ya mchezaji huyo wa miaka 22 kutoshiriki mechi ya wakubwa, huku Bristol City ikitafakari kubadili mkataba wake wa mkopo na kuufanya wa kudumu. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kasey Palmer

Meneja wa zamani wa Borussia Dortmund Peter Stoger, ambaye amekuwa nje ya kazi tangu alipoondoka Ujerumani mwezi Mei mwaka jana, anapigiwa upatu kuchukua nafasi hiyo kwa mkataba wa kudumu. (Leicester Mercury)

Bora kutoka Jumatatu

Rais wa Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi amesisitiza kuwa klabu hiyo haitamuuza mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymar, 27, na Kylian Mbappe mwaka huu. (Marca)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Neymar na Kylian Mbappe

Meneja wa zamani wa Chelsea na Manchester United Jose Mourinho anaamini kuwa kiungo wa kati wa Ubelgiji Eden Hazard atafanya vyema Real Madrid endapo ataamua kuhamia klabu hiyo ya Uhispania. (London Evening Standard)

Arsenal huenda isimpate Marc Overmars kama mkurugenzi wa kiufundi kwasababu Ajax amekataa kumuachilia na haiko tayari kulipwa ofa yoyote, kwa mujibu wa ripoti. (Sun)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii