Kepa Arrizabalaga: 'Hujuma kwa Chelsea' baada ya kipa kukataa agizo la Maurizio Sarri katika fainali ya Carabao

Maurizio Sarri and Willy Caballero Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maurizio Sarri alikuwa anataka kumuingiza Willy Caballero

Je umewahi kuhsuhudia kitukama hichi?

Mchezaji akataa kuondoka uwanjani - na meneja wake apoteza muelekeo wa mechi.

Kipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga alikataa jitihada za meneja Maurizio Sarri kumbadilisha uwanjani katika dakika za ziada za mechi ya fainali ya kombe la Carabao, hatua iliomuacha meneja huyo akiwa na hasira kubwa nje ya uwanja huo.

Arrizabalaga alikuwa amehudumiwa kwa kubanwa kwa maumivu ya msuli, na wakati mechi ikiwa 0-0, Sarri alikuwa anajitayarisha kumuingiza kipa wa akiba Willy Caballero katika nafasi ya Kepa kabla ya awamu ya mikwaju ya penalti.

Lakini baada ya kunyosheana vidole kwa muda kadhaa na kupiga kelele, HAPANA!, ilibidi Sarri asalimu amri.

Refa Jonathan Moss alikimbia kumfuata Sarri kuthibitisha iwapo kweli anataka Arrizabalaga aondoke au la, na Sarri, ilibidi abadili msimamo wake kabla ya kuondoka kwa hasira , na muda mfupi baadaye kurudi, akimuacha kipa wa akiba Caballero akiwa amechanganyikiwa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mlinzi wa Chelsea David Luiz ajaribu kumtuliza Kepa Arrizabalaga uwanjani

Arrizabalaga alifanikiwa kuokoa mkwaju wa Leroy Sane - lakini Raheem Sterling alifunga bao la ushindi katika mikwaju hiyo ya penalti wakati Manchester City walipotuzwa mabingwa wa taji hilo la Carabaokwamwaka wa pili kutokana na ushindi wa mwisho wa mabao 4-3.

Sarri hakuonekana kuonyesha hisia zozote, wakati wachezaji wake wakionekena kuhuzunishwa kwa kushindwa.

'Ni hujuma kwa Chelsea' - uchambuzi

Aliyekuwa mshambuliaji huko Stamford Bridge Chris Sutton ameeleza matukio ya jana kama ''hujuma kwa Chelsea" na kuapa kwamba Arrizabalaga "hastahili kucheza tena katika klabu hiyo".

Hilo linajiri kufuatia wiki kadhaa za uvumi kuhusu nafasi ya Sarri kama meneja wa klabu hiyo na wasiwasi kuhusu mbinu zakezilizopewa jina maarufu "sarri-ball".

"Kama ningekuwa Sarri ningeondoka. Huwezi kudharauliwa. Ni kwanini wachezaji hawakumburura Kepa nje?

"Kepa anastahili kufutwa kazi, sio Sarri. Amedhauriliwa - sio jambo zuri kwa meneja."

Aliyekuwa mchezaji wa England na timu ya Tottenham Jermaine Jenas anasema ni wazi "hakuna heshima" kwa meneja, lakini amesema Sarri ameonyesha "hana ustaarabu" kwa kuamua kuondoka uwanjani baada ya kushindwa.

Mambo yalivyoitukia...

Haki miliki ya picha PA
Image caption Kipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga abanwa na maumivu ya msuli karibu mwisho wa muda wa ziada
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kipa wa akiba Willy Caballero yuko tayari kuingia uwanjani
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Arrizabalaga ampigia kelele meneja wake, hataki kuondoshwa uwanjani
Haki miliki ya picha PA
Image caption Maurizio Sarri amjibu kwa hasira Arrizabalaga huku msaidizi wake Gianfranco Zola akishangazwa
Haki miliki ya picha PA
Image caption Refa Jonathan Moss amuuliza Sarri iwapo anataka kumtoa kipa wake
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sarri anaondoka uwanjani na kipenga kinapulizwa kumalizika muda wa ziada

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii