Kepa Arrizabalaga: Kipa wa Chelsea ametozwa faini na kutakiwa aombe msamaha kwa mkasa wa Wembley

Kepa Arrizabalaga
Maelezo ya picha,

Chelsea ilimsajili Kepa Arrizabalaga kutoka Athletic Bilbao kwa kitita cha £71m mnamo Agosti 2018

Kipa Kepa Arrizabalaga ametozwa faini ya thamani ya mshahara wa wiki moja na ameomba msamaha kwa kukataa kuondolewa uwanjani wakati a mechi ya fainali ya taji la Carabao wakati timu hiyo ilipofungwa na Manchester City Jumapili.

Mchezaji huyo raia wa Uhispani alikataa akuondolewa uwanjanai na kipa wa ziada Willy Caballero kuichukua nafasi yake katika uwanja wa Wembley.

"Licha ya kwamba hatukuelewana, kwa kujitathmini, nilifanya makosa kwa namna nilivyoshughulikia hali hiyo ," Kepa amesema katika taarifa rasmi ya Chelsea.

Meneja Maurizio Sarri amesema kwamba yeye na Kepa wamekuwa "na mazungumzo mazuri".

Sarri, aliyeondoka kwa hasira wakati Kepa alipokataa kutoka uwanjani kuikia dakika za mwisho za muda wa ziada , pia amebaini kwamba 'hawakuelewana'.

Lakini aliongeza: "Kepa ametambua alifanya makosa makubwa katika namna alivyofanya.

"Ameniomba msamaha, amewaomba wachezaji wenzake na timu nzima kwa jumla msamaha. Ni uamuzi wa klabu hiyo iwapo watataka kumuadhibu kwa mujibu wa sheria za klabu, lakini binafsi, suala hili limemalizika.

Maelezo ya picha,

Maurizio Sarri alikuwa anataka kumuingiza Willy Caballero

"Uchezaji wa timu nzima kwa jumla, ulikuwa ni matumaini makubwa na ni aibu kuona namna tukio hili limegubika mchezo wa na jitihada za timu katika fainali iliyokuwana ushindani mkubwa."

Kepa, ambaye ni mchezaji wa klabu hiyo aliyesajiliwa kwa kitita kikubwa £71m, alikaidi jitihada za Sarri kumuondosha uwanjani na kumuweka kipa mwenza Caballero kabla ya Manchester City kushinda kwa penalti. Raia huyo wa Italia alionekana na haisra kubwa na aliondoka uwanjani kabla ya muda mfupi kurudi tena.

Mchezahi huyo wa miaka 21 wa zamani wa Athletic Bilbao amesema: "Nilitaka kuchukua fursa leo kuomba radhi kikamilifu na binafsi kwa kocha, kwa Willy, wachezaji wenzangu na timu nzima kwa jumla.

"Nimelifanya hili na sasa nataka kuomba radhi kwa mashabiki pia. NItajifunza kutokana na mkasa huu na nitakubali adhabu yoyote itakayoamua klabu dhidi yangu."

Timu hiyo itatoa fedha atakazotoa Kepa katika faini hiyo kama msaada kwa wakfu wa Chelsea.