Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 27.02.2019: De Gea, Higuain, Rakitic, Monchi, Cardoso

David de Gea Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption David de Gea

Kipa wa Uhispani David de Gea, 28, anakabiliwa na hatari ya kushuka thamani nje ya Manchester United, licha ya klabu hiyo kuwa tayari kumpatia mkataba mpya wa euro £350,000 kwa wiki. (Evening Standard)

Manchester United inamfuatilia kiungo wa kati wa Barcelona na Croatia Ivan Rakitic, 30. (Mail)

Juventus haina mpango wa kumrudisha tena mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Gonzalo Higuain katika klabu hiyo mkataba wake wa bure utakapokamilika Chelsea. (Il Corriere di Torino, via Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gonzalo Higuain (kulia)

Roma wamekubaliana na uamuzi wa kuondoka kwa meneja wao wa kiufundi Monchi, huku Arsenal ikiongoza katika kampeini ya kumuajiri mhispania huyo wa miaka 50 msimu huu. (Evening Standard)

Watford ni miongoni mwa vilabu vinavyomwania mlinzi wa Boavista Goncalo Cardoso, 18. (Mail)

Ndugu wa mlinzi wa Chelsea Antonio Rudiger amesema mhispania Cesar Azpilicueta, 29, anastahili kuvuliwa kwa wadhifa wa unahodha na kupewa ndugu yake. (Mirror)

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Cesar Azpilicueta(kulia)

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa anayechezea timu ya wachezaji wa chini ya miaka 21 amekuwa akifuatiliwa na Everton. (Mail)

West Brom wanamfuatilia mlinzi wa Crawley Town David Sesay, 20. (Sun)

Kipa wa Ajax na Cameroon Andre Onana, 22, yuko katika orodha ya kuwa kipa mpya wa Barcelona endapo Jasper Cillessen, 29, ataondoka klabu hiyo. (El Club de la Mitjanit, via Sport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Andre Onana

Meneja wa Bradford Park Avenue Mark Bower ni anapigiwa upatu kuajiri na klabu ya Bradford City. (Telegraph & Argus)

Tetesi Bora kutoka Jumanne

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri alimgombeza kipa Kepa Arrizabalaga kwa kupuuza amri yake ya kumtaka kutoka uwanjani wakati wa finali ya kombe la Carabao. (Sun)

Kisa hicho kiliwafanya wachezaji wengi wa Chelsea kumkasirikia kipa huyo wa miaka 24 raia wa Uhispania. (Daily Express)

Haki miliki ya picha Getty Images

Arsenal inaongoza katika kinyang'anyiro cha kumuwania beki wa kulia wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka,21, na iko tayari kufikia bei ya euro milioni 40 iliyoitishwa na klabu yake. (Sun). (Sun)

Mmiliki wa Leeds United Andrea Radrizzani huenda akalazimika kuuza klabu hiyo endapo itashindwa kupanda ngazi ya kushiriki ligi ya primia. (Daily Mail)

Manchester United na Chelsea wanamnyatia nahodha wa AC Milan Alessio Romagnoli.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii