Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 09.03.2019: Neymar, Guardiola, Pochettino, Marcelo, Felix, Monchi

Neymar Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Neymar

Real Madrid ina mpango wa kumnunua mchezaji nyota wa Brazil, Neymar, 27 kutoka Paris St Germain kwa kima cha euro milioni 300 (£259m). (Sport)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amekubali kujaza pengo la Massimiliano Allegri anayechezea Juventus, baada ya tetesi kuibuka kuwa Cristiano Ronaldo huenda akaondoka mji wa Turin. (Radio CRC - via Mirror)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino amesema kuwa angelipendelea sana kurudi Uhispania kufanya kazi ya ukocha na lengo lake ni kujiunga na Real Madrid hasa baada ya rekodi yake nzuri ya Spurs. (ESPN)

Beki wa kushoto wa Real Madrid, Marcelo amekubaliana na masharti ya mkataba wa miaka minne ya kujiunga na Ronaldo katika klabu ya Juventus. (La Stampa, via Calciomercato)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Marcelo(kulia)

Arsenal imepiga hatua katika juhudi za kumsajili Monchi kama meneja wao mpya wa kiufundi baada ya Roma kutangaza kuwa mhispania huyo ameondoka kalabu hiyo

Monchi mwenye umri wa miaka 50 aliwahi kufanya kazi na meneja wa Gunners Unai Emery akiwa Sevilla. (Telegraph)

Manchester United wanamnyatia mlinzi wa Benfica na Ureno Ruben Dias, 21, wanapojiandaa kuimarisha safu yao ya ulinzi msimu huu wa joto. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ruben Dias(Kulia)

Wolves imewapatia maafisa wake jukumu la kufuatilia mchezo wa kiungo wa kati wa Benfica Joao Felix 19, atakashiriki mchuano wa kombe la Uropa. (Birmingham Mail)

Leeds United wanamfuatilia kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Luke Freeman, 26 anayechezea QPR . (Talksport)

Ole Gunnar Solskjaer ameonesha mpango wa kutegemea ushirikiano wa Marcus Rashford na Romelu Lukaku katika safu ya mashambulizi ya Manchester United. (Manchester Evening News)

Haki miliki ya picha Getty Images

Kiungo wa kati wa West Ham Felipe Anderson, 25, amesma anataka kusalia London Stadium ili apate kuwa shujaa wa klabu hiyo kama mshambuliaji wa Italia Paolo Di Canio. (London Evening Standard)

Meneja wa Crystal Palace Roy Hodgson,71 ambaye ni meneja wa mzee zaidi katika historia ya ligi ya Primia amesisitiza kuwa hana mpango wa kustaafu hivi karibuni. (Sky Sports)

Hodgson anaamini beki wa kulia na kushoto wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka, ataipatia England umuhimu katika hatima yake ya siku zijazo ya soka ya kimataifa badala ya DR Congo. (Times - subscription required)

Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Roy Hodgson, meneja mzee zaidi katika historia ya ligi ya Primia

Bayern Munich wanakaribia kukamilisha mpango wa kumsajili Nicolas Pepe kutoka Lille.

Barcelona na Paris St-Germain pia wanamnyatia winga huyo wa kimataifa wa Ivory Coast, 23. (Le10 Sport)

Haki miliki ya picha Getty Images

Barcelona imehusishwa na uhamisho wa kiungo wa kati wa Sochaux Lucien Agoume, 17. (Mundo Deportivo)

Mshambuliaji wa Tottenham na Korea Kusini Son Heung-min, 26, anakubaliana na baba yake mzazi kuwa asioe mke hadi pale atakapostaafu kucheza soka. (Guardian)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii