Cristiano Ronaldo: Mshambuliaji wa Juventus aonesha umahiri wake katika ligi ya mabingwa

Cristiano Ronaldo celebrates Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 13 Juventus imepita hatua ya muondoano katika ligi ya mabingwa

Cristiano Ronaldo alisajiliwa ili kuipatia Juventus ushindi wa ligi ya mabingwa - na huenda akafanikisha ndoto hiyo.

Nyota huyo raia wa Ureno alionesha umahiri wake katika soka ya barani ulaya baada ya kuiwezesha klabu hiyo ya Italia kufuzu katika hatua ya robo fainali baada ya kuinyuka Atletico Madrid.

Kulikuwa na hofu huenda Juve huenda ikaondolea katika hatua ya muondowano baabda ya kufungwa mabao mawili katika awamu ya kwanza ya michono hiyo.

Ronaldo alikuwa anakabiliwa na uwezekano wa kushindwa kufika angalau nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010 - na mara ya pili katika misimu 12.

Lakini hivi ndivyo mambo yalivyokuwa ...

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Ronaldo alifunga bao la kwanza katika dakika ya 27 baada ya kuruka juu zaidi ya mlizi wa Atletico Juanfran na kuipatia Juvematumaini ya kubadilisha mkondo wa mchezo wao wa awali ambapo walifungwa 2-0
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Dakika nne baada ya muda wa mapumziko, alifunga bao la pili - dhidi ya timu ambayo haijawahi kufungwa katika mechi tano zilizopita.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakati Federico Bernardeschi alipolemewa kupenya lango la Atletico na Angel Correa, ni mtu mmoja tu alingeliweza kufanya miujiza ya katka dakika nne za mwisho za kuamua nani atakaye fuzu kwa robo fainali
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Juventus ikishangilia ushindi wao dhidi ya Atletico Madrid

Ushindi huu wa sasa unamaanisha:

  • Ronaldo amefunga jumla ya mabao 124 katika mashindano ya vilabu bora vya soka barani ulaya - Ushindi huu umefungua pengo la mabao 18 dhidi ya Lionel Messi katika orodha ya wafungaji bora wa mabao.
  • Ronaldo amefunga hat-tricks nane katika Champions League.
  • Ronaldo anasalia katika nafasi ya kuongeza ushindi wake wa mara tano wa taji la Champions League- Ni nyota wa zamani wa Real Madrid Francisco Gento, ambaye ameshinda vikombe vingi Ulaya.
  • Ina karibu miaka minne tangu timu inayomjumuisha Ronaldo imekaribia kuondolewa katika Champions League lakini akabadilisha mkondo wa mchezo na kushinda kwa mara ya nne mtawalio.

'Hii ndio sababu wamenileta hapa'

Ronaldo alijiunga na Juventus kutoka Real Madrid msimu uliyopita kwa kima cha euro milioni 99.2 na kuandikisha rekodi ya uwa mchezaji wa soka anayelipwa feha nyingi zaidi.

Jukumu lake kubwa lilikuwa kuisaidia kablu hiyo ya Turin kushinda ligi ya mabingwa.

"Hii ndio sababu Juventus ilinileta hapa, ili kusaidia kufanya vitu ambavyo havijawahi kufanywa," alisema Ronaldo, ambaye sasa amefunga mabao 18 katika mechi 14 za hatua ya muondoano katika ligi ya mabingwa.

"Ilikuwa usiku maalum kwa timu yetu bila na bila shaka imekuwa hivyo .

"Ari hii inahitajika ili kushinda Champions League. Tulifurahia mchezo wetu. Atletico ilikuwa timu kali lakini sisi pia tulikuwa imara. Tunasubiri kuona kile kitakachofanyika."

Haki miliki ya picha Juventus FC Twitter
Image caption Wachezaji wa Juventus wakishangilia ushindi wao dhidi ya Atletico

Rio Ferdinand, mchezaji wa mwenza wa Ronaldo walipokuwa pamoja Manchester United, ameiambia BT Sport: "Cristiano atasalia kuwa 'mbabe' wa soka kile alichofanya ni kitu cha kushangaza.

"Katika ligi ya mabingwa amevunja rekodi zote. Na sasa ameshinda Atletico timu inayosifika kwa kuwa na ulinzi mkali."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii