Tetesi za soka Ulaya: De Gea, Courtois, Eriksen, Bale, Sessegnon, Icardi, Perisic

Real Madrid inamsaka Muhispania David de Gea, mwenye umri wa miaka 28 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zinedine Zidane anamtaka Muhispania David de Gea, mwenye umri wa miaka 28

Real Madrid inataka kusaini mkataba na mlinda lango wa Manchester United Muhispania David de Gea, 28,kufuatia kurejea kwa Zinedine Zidane kwenye klabu hiyo. (Sunday Mirror)

Zidane anasema hakuna uamuzi uliochukuliwa juu ya hatma ya siku za usoni ya mlinda lango wa Mbelgiji Thibaut Courtois katika klabu hiyo. Thibaut Courtois mwenye umri wa miaka 26 ambaye alisaini mkataba na klabu hiyo baada ya Zidane kuondoka mwezi Mei 2018, aliondolewa kwenye mechi ya kwanza tu baada ya Zidane kurejea. (Evening Standard)

Madrid pia wanamuwania mchezaji wa safu ya kati wa Tottenham Christian Eriksen - lakini klabu hiyo ya Primia Ligiinataka pauni £200m kwa ajili ya Dane mwenye umri wa miaka . (Sunday Star)

Real wanaweza kumuuza mchezaji wa safu ya mashambulizi kutoka Wales Gareth Bale, mwenye umri wa miaka 29, kwa Chelsea kama sehemu ya mpango wa kubadilishana mchezaji wa Ubelgiji Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 28 anayecheza safu ya kati. (Sunday Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tottenham wana haja sana na winga wa Fulham Ryan Sessegnon

Chelsea watajaribu kuzuwia ndoto ya kijana Callum Hudson-Odoi mwenye umri wa miaka 18-ya kuhamia Bayern Munich, ikiwa Hazard ataamua kuhamia Real Madrid. Washindi hao wa Championi ya Ujerumani wanaweza kuvunja rekodi ya malipo ya wachezaji katika Primia Ligi kama winga huyo atapenda kwenda Bundesliga. (Sun)

Tottenham wanajiandaa kumnunua winga wa Fulham Ryan Sessegnon mwa pauni milioni £50m . Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 ambaye Manchester United na Paris Saint-Germain - wameonyesha nia ya kumtakabado hajasaini mkataba na Fulham. (Sunday Mirror)

Mauricio Pochettino pia aliutuma ujumbe kujaribu kumshawishi mchezaji wa safu ya mashambulizi wa timu ya Ureno ya Benfica mwenye umri wa miaka 19 Joao Pedro Neves Filipe kujiunga nao. (Sunday Star)

Inter Milan wako tayari kumchukua mshambuliaji wa Argentine Mauro Icardi, mwenye umri wa miaka 26, pamoja na kiungo katika safu ya mashambulizi ya Croasia Ivan Perisic,ambaye ana umri wa miaka 30, huku Manchester United na Arsenal kwa pamoja wakionyesha haja ya kusaini mkataba na yeyote kati ya wachezaji hao. (La Gazzetta Dello Sporto - in Italian)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Inter Milan wako tayari kumchukua mshambuliaji wa Argentine Mauro Icardi

Paris St-Germain wamesitisha mazungumzo ya mkataba na mlinda lango wa Italia Gianluigi Buffon, mwenye umri wa miaka 41, mchezaji wa safu ya kati kulia Dani Alves, mwenye umri wa miaka 35, pamoja na mlinzi kutoka Brazil Thiago Silva, mwenye umri wa miaka 34, baada ya klabu hiyo ya Ufaransa kutupwa nje ya Championi Ligi na Manchester United. (L'Equipe - in French)

Meneja wa zamani wa Tottenham Harry Redknapp anaamini Mauricio Pochettino ana "ndoto" ya kazi yake na kwamba haoni kwingine bora zaidi anakoweza kwenda kuzuri zaidi ya kuwa meneja wa Tottenham". Pochettino alikuwa amehusishwa na kazi hiyo katika klabu ya Real Madrid au Manchester United. (Star)

Meneja Pep Guardiola anasema kuwa winga wa klabu ya Uingereza ya Borussia Dortmund Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 18, "hakutaka changamoto " ya kujaribu kuwa mchezaji wa kwanza wa kawaida wa Manchester City. Sancho aliondoka katika klabu hiyo ya Primia Ligi Agosti 2017. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Pep Gardiola anasema Sancho hakuweza kukabiliana na changamoto ya kuwa mchezaji wa kawaida katika Manchester City

Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo inataka kumshawishi mlinzi wa klabu ya Uingereza ya Crystal Aaron Wan-Bissaka kuchezea timu ya taifa hilo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21-aliyezaliwa London ana asili ya Kongo. (Independent)

Arsenal wako makini kusaini mkataba na Wan-Bissaka, ingawa Palace wanamtaka kwa pauni £40m arejee mara moja. (Sun)

Meneja wa Everton m Marco Silva amemuambia mlinzi Yerry Mina raia wa Colombia, mwnye iumri wa miaka 24, kuwa anahitaji kuwa wa kuamika , kama anataka kuwa mchezaji wa kawaida wa timu hiyo. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo inataka kumshawishi mlinzi wa klabu ya Uingereza ya Crystal Aaron Wan-Bissaka kuchezea timu ya taifa hilo

Manchester United, Tottenham na Manchester City wameazimia kusaini mkataba na mchezaji wa kiungo cha kati kutoka klabu ya Ufaransa ya Lyon Tanguy Ndombele mwenye umri wa miaka 22. (Calciomercato)

Barcelona wanamtaka mshambuliaji timu ya Celta Vigo ya nchini Uruguay -Maxi Gomez - lakini huenda wasimchukue huyo mwenye umri wa miaka 22- kwasababu hana paspoti ya EU.(Marca - in Spanish)

Sevilla imeanza mazungumzo na mkurugenzi wa zamani wa timu ya soka ya Roma football Monchi, ambaye amekuwa akishukiwa kuhamia Arsenal. (Talksport)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema klabu yake haihitaji "kumnunua mchezaji yeyeote kwa pesa nyingi ". (Sunday Times - subscription required)

Mchezaji wa safu ya mashambulizi ya kati wa Everton Mbrazilian Richarlison,mwenye umri wa miaka 21, anasema nusura aache soka alipokuwa kijana na badala yake "auze ice creams" ili kuisaidia familia. (Liverpool Echo)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii