Cristiano Ronaldo: Mshambuliaji wa Juventus achukuliwa hatua na Uefa kwa 'kushangilia' bao

Mshambuliaji wa Juventus , Cristiano Ronaldo Haki miliki ya picha EPA
Image caption Ronaldo amefunga mabao 124 katika ligi ya mabingwa

Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo amechukuliwa hatua za kinidhamu na Uefa baada ya kushangilia 'visivyo' ushindi wa klabu yake dhidi ya Atletico Madrid katika mchuano wa ligi ya mabingwa wa kufuzu kwa awamu ya robo fainali juma lililopita.

Nyota huyo wa 34 alionekana kumkejeli meneja wa Atletico, Diego Simeone, huku akiwageukia mashabiki wa klabu hiyo na kujishika sehemu zake za siri.

Ronaldo alifanya kosa hilo wakati akishangilia hat-trick yake iliyoifanya Juventus kuishinda Atletico mabao 3-0.

Uefa itatoa uamuzi wa kesi hiyo Machi 21.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Cristiano Ronaldo

Simeone amepigwa faini ya pauni ya 17,000 kwa kushangilia.

Juventus itamenyana na Ajax katika mechi ya robo fainali.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii