Tetesi za soka Ulaya Jumanne 19.03.2019: Mane, Messi, Ronaldo, Beckham, Sanchez, Suarez

Mkufunzi wa Real madrid Zinedine Zidane Haki miliki ya picha Getty Images

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane anataka kumsaini mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane ,26, mwisho wa msimu huu. (France Football)

Manchester United huenda ikamsajili beki wa Roma na Ugiriki Kostas Manolas, 27, kwa kwa bei ya mashauriano mwisho wa msimu huu . Manolas anazuiliwa kuondoka katika klabu hiyo na kifungu cha sheria cha £30.8m katika kanbdarasi yake (Calciomercato, via Manchester Evening News)

David Beckham ana ndoto za kumsajili nyota wa Barcelona's Lionel Messi, 31, ama mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo, 34, katika timu yake ya Inter Miami iliopo nchini Marekani. (Fox Sports)

Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez amepokea ofa ya kumuongezea kandarasi yake katika klabu hiyo baada ya msimu huu . (Chronicle)

Mshambuliaji wa Manchester United Alexis Sanchez, 30, huenda akajiunga na Juventus mwisho wa msimu huu , iwapo raia huyo wa Chile atakubali kupunguza mshahara wake wa £500,000 kwa wiki. (Calciomercato, via Express)

United inafikiria kumruhusu kiungo wa kati wa Brazil Andreas Pereira, 23, kuondoka kwa mkopo kwa kipindi chote cha msimu ujao ili kupata uzoefu. (Sun)

Arsenal inalenga kumnunua mchezaji wa Portugal Gelson Martins. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa sasa yuko kwa mkopo katika ligi ya daraja la kwanza Monaco kutoka Atletico Madrid.(A Bola, via Talksport)

Arsenal itamrudisha kiungo wa kati wa Uhispania Denis Suarez, 25, katika timu ya Barcelona mwisho wa msimu huu baada ya kushindwa kumvutia mkufunzi Unai Emery. (sun)

Haki miliki ya picha Getty Images

Shirikisho la soka nchini Ujerumani limetembelea uwanja wa Uingereza wa St George's Park ili kupata mawazo mapya ya kujenga uwanja wao mpya wa mazoezi na pia wamekuwa wakiuliza kuhusu ukufunzi pamoja na kuwaimarisha wachezaji.(Mirror)

Liverpool na Newcastle zinamnyatia kinda wa Middlesbrough mwenye umri wa miaka 18 Bilal Brahimi, ijapokuwa klabu ya daraja la kwanza ya Rennes pia inamtaka raia huyo wa Ufaransa. (Teamtalk)

Bournemouth inataka kumsaini kiungo wa kati wa Uingereza na Chelsea mwenye umri wa miaka 20 Mason Mount, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Derby ambapo ana kandarasi ya muda mrefu kwa msimu wa 2019-20. (Sun)

Beki wa zamani wa Manchester United Nemanja Vidic anaamini kwamba klabu hiyo inafaa kumsaini kiungo wa kati mwisho wa msimu huu . (Express)

Aliyekuwa mshambuliaji wa Chelsea Tony Cascarino anaamini kwamba mshambuliaji wa Newcastle Salomon Rondon, ambaye yuko kwa mkopo kutoka West Brom amekuwa mchezaji bora aliyesainiwa katika ligi ya Uingereza msimu huu. (Talksport)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii