Tetesi za soka Ulaya Jumatano 20.03.2019: Griezmann, Hazard, Ibrahimovic, Dybala, Rabiot, Manolas

Antoine Griezmann

Manchester United inapigiwa upatu kumsaini mshambuliaji wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, 27,mwisho wa msimu huu . (Sport, via Manchester Evening News)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard, 27, anasema kuwa hatoathiriwa na uvumi kwamba atajiunga na Real Madrid mwisho wa msimu huu.. (Metro)

Mshambuliaji wa Los Angeles Galaxy Zlatan Ibrahimovic, 37, amefichua ni kwa nini alikataa kujiunga na Manchester City kabla ya kujiunga na Manchester United 2016. (Mirror)

Liverpool huenda ikawa tayari kutia saini makubaliano ya kumsajili raia wa Argentina Paulo Dybala, 25, kutoka Juventus katika kipindi cha wiki chache zijazo. (Tutto Mercato, via Team Talk)

Manchester United bado ina fursa ya kumsaini kiungo wa kati wa PSG mwenye umri wa miaka 23 Adrien Rabiot baada ya mamake ambaye pia ni ajenti wake kukana habari kwamba mchezaji huyo wa Ufaransa amekubali kujiunga na Barcelona (L'Equipe, via Metro.

Haki miliki ya picha Getty Images

Manchester United ama Arsenal huenda wakamsajili beki wa Roma na Ugiriki Kostas Manolas kwa dau la chini mwisho wa msimu huu. Kifungu cha sheria ya kuondoka katika klabu hiyo hakitafanya kazi iwapo klabu yake haitafuzu katika kombe la vilabu bingwa Ulaya.. (Calciomercato, via Mirror)

Kipa Loris Karius, 25, ameiomba Liverpool kufutilia mbali makubaliano ya mkopo wa miaka miwili na klabu ya Besiktas. (Turkiye Gazetesi, via Liverpool Echo)

Wolves ina hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Ureno wa timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 19 Francisco Trincao, 19, kutoka Braga. (Birmingham Mail)

Mahitaji ya mshahara wa Olivier Giroud mwenye umri wa miaka 32 yanaweza kumfanya kuwa mchezaji ghali zaidi katika klabu za Marseille au Lyon. (Le10 Sport - in French)

West Ham na Newcastle United zinamchunguza mshambuliaji wa klabu ya Mainz Erkan Eyibil. Mchezaji huyo mwenuye umri wa miaka 17 kutoka Uturuki ametajwa kuwa 'Mesut Ozil' mpya (Turkish Football)

Beki wa Paris St-Germain na Brazil Dani Alves, 35, amekubali kuongezewa kandarasi yake na mabingwa hao wa Ufaransa . (ESPN)

Kipa wa Manchester City Curtis Anderson, 18, ambaye alikuwa katika kikosi cha Uingereza kilichoshinda kombe la dunia la 2017 miongoni mwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 amejiunga na klabu ya Charlotte Independence nchini Marekani . (Daily Mail)

Mkufunzi mpya wa klabu ya Leicester Brendan Rogers anasema kuwa anatarajia beki wa Croatia Filip Benkovic ataichezea klabu yake msimu ujao.

The Foxes walimuuza kwa mkopo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kwa klabu ya Celtic mwisho wa msimu uliopita na Rodgers alifanya kazi naye pamoja katika klabu hiyo kabla ya kujiunga na Leicester.(Leicester Mercury)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii