Callum Hudson-Odoi: Ghana yamkosa winga wa Chelsea baada ya kuitikia wito wa Uingereza

Callum Hudson Odoi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Hudson-Odoi ameifungia Chelsea magoli matano msimu huu

Winga wa Chelsea Callum Hudson-Odoi - ambaye hajaanzishwa mechi yoyote ya ligi ya Premia anasema kuwa ameshangazwa baada ya kupata wito katika timu ya Uingereza.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 alishirikishwa katika kikosi cha timu ya Uingereza siku ya Jumatatu kwa maandalizi ya mechi za kufuzu kwa michuano ya Yuro 2020 dhidi ya Jamhuri za Czech na Montenegro.

Ameichezea Chelsea mara 19 msimu huu na kufunga magoli matano.

''Sio jambo la kawaida kwangu lakini nafurahia sana'' , Hudson Odoi alisema. ''Nilidhani meneja alikuwa akifanya mzaha''.

Alikuwa na timu ya Uingereza iliopo na wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21, baada ya kupata mwaliko wake wa kwanza wiki iliopita, ambapo aliambiwa kwamba ataichezea timu kubwa na mkufunzi wa kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Aidy Boothroyd.

''Nilishangaa sana na nilipoambiwa kwamba nimepandishwa hadi timu kuu sikuamini'', Hudson Odoi aliongezea.

Hudson Odoi alishirikishwa katika kikosi hicho baada ya Luke Shaw, John Stones , Fabian Delph na Ruben Loftus Cheek kujiondoa.

Uingereza itacheza dhidi ya Czech katika uwanja wa Wembley siku ya Ijumaa, 22 Machi na wataelekea Montenegro siku ya Jumatatu , 25 Machi.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mizizi ya Callum James Hudson Odoi

Alizaliwa tarehe 7 mwezi Novemba 2000 kutoka kwa wazazi wake Bwana na bi Bismark Odoi katika eneo la Uingereza la Wandsworth .

Ni mtoto wa pili katika wavulana watatu.

Familia ya Callum Hudson ina mizizi ya taifa la Ghana. Babaake Bismark Odoi ni mchezaji wa zamani wa klabu ya Ghana Hearts of Oak .

Hudson-Odoi ameichezea Uingereza mara 23 na atakuwa mchezaji wa nane mwenye umri mdogo wa taifa hilo iwapo ataanzishwa dhidi ya jamhuri ya Czech ama Montenegro.

Theo Walcott ndiye aliyekuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi.

Alikuwa na umri wa miaka 17 na siku 75 wakati alipoichezea timu hiyo dhidi ya Hungary kwa mara ya kwanza 2006 baada ya kukosa kucheza katika ligi kuu.

Mechi 11 kati ya 19 alizoshiriki Hudson Odoi akiichezea Chelsea msimu huu alicheza kama mchezaji wa ziada huku akianzishwa katika mechi za mashindano ya makombe.

Katika mechi nane alizoanza, hatahivyo amefunga magoli manne na kutoa pasi nne zilizosaidia kufungwa kwa magoli.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Hudson-Odoi kushoto na Declan Rice kulia

Chelsea yakataa kumuuza

Akikasirishwa na muda aliopewa kucheza mechi katika klabu ya Chelsea.

Hudson Odoi aliomba uhamisho mwezi Januari kufuatia hamu ya dau la £35m kutoka kwa Bayern lakini Chelsea ilikataa kumuuza.

Mapema mwezi huu , mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri alisema kuwa ni hatari kumweka katika shinikizo kinda huyo akisema kuwa atakuwa mchezaji mzuri atakapofikisha umri wa miaka 22 au 23.

Kikosi cha Uingereza

Kipa: Jack Butland (Stoke City), Tom Heaton (Burnley), Jordan Pickford (Everton)

Mabeki: Trent Alexander-Arnold (Liverpool), Ben Chilwell (Leicester City), Michael Keane (Everton), Harry Maguire (Leicester City), Danny Rose (Tottenham Hotspur), James Tarkowski (Burnley), Kieran Trippier (Tottenham Hotspur), Kyle Walker (Manchester City)

Viungo wa kati : Ross Barkley (Chelsea), Dele Alli (Tottenham Hotspur), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Jordan Henderson (Liverpool), Declan Rice (West Ham), James Ward-Prowse (Southampton), Callum Hudson-Odoi (Chelsea)

Washambuliaji: Harry Kane (Tottenham Hotspur), Marcus Rashford (Manchester United), Jadon Sancho (Borussia Dortmund), Raheem Sterling (Manchester City), Callum Wilson (Bournemouth)

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii