Vilabu bingwa Afrika: Simba ya Tanzania na Gor Mahia ya Kenya zapewa wapinzani

Kikosi cha simba kilichoshriki mechi dhidi ya Vita Club

Droo ya kombe la Vilabu bingwa barani Afrika hatimaye imetolewa.

Katika michuano hiyo klabu ya Simba kutoka nchini Tanzania imepangwa kucheza dhidi ya mabingwa wa zamani wa kombe hilo TP Mazembe wa DR Congo huku mabingwa wa ligi ya Kenya Gor Mahia wakimenyana dhidi ya klabu ya S Berkane kutoka Morocco.

Droo hiyo iliofanyika siku ya Jumatano katika mji wa mkuu wa Misri, Cairo iliwakutanisha mabingwa hao huku safari ya michuano hiyo ikielekea kufika ukingoni.

Baadhi ya magwiji wa kandanda waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na naibu katibu mkuu wa CAF Anthony Baffoe, chini ya usaidizi wa mshambuliaji wa zamani wa Cameroon Patrick Mboma pamoja na Emad Moteab kutoka Misri.

Pia baadhi ya waliohudhuria walikuwa wawakilishi wa vilabu vinavyoshiriki.

Jinsi Simba na Gor Mahia zilivyotinga robo fainali

Katika hatua ya kuelekea robo fainali klabu ya Simba ya Tanzania ilivunja mwiko wa miaka 25 baada ya kuilaza klabu ya Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kwa goli 2-1, ushindi uliowapatia alama 9 baada ya kucheza mechi sita.

Haki miliki ya picha Sportpesa

Hiyo ilikuwa ni mara ya pili kwa Simba kufuzu robo fainali, mara ya kwanza ikiwa miaka 45 iliyopita mnamo 1974 ambapo walisonga mpaka kufikia hatua ya nusu fainali na kutolewa na Ghazl Al-Mahalla ya Misri kwa mikwaju ya penati 3-0.

Nayo klabu ya Kenya Gor Mahia ilijipatia tiketi ya kufuzu robo fainali ya michuano hiyo baada ya kuilaza klabu ya Petro Atletico ya Angola 1-0 katika mechi kali ya CAF wakiwa na wachezaji 9 pekee bila mkufunzi wake Hassan Oktay katika eneo la kiufundi.

Bao la pekee lilifungwa na raia wa Rwanda Jacques Tuyisenge.

Droo ya Total CAF Confederation Cup

Nkana (Zambia) vs CS Sfaxien (Tunisia)

Etoile du Sahel (Tunisia) vs El Hilal (Sudan)

Hassania Agadir (morocco) vs Zamalek (Egypt)

Gor Mahia (Kenya) vs RS Berkane (Morocco)

CS Constantine (Algeria) vs Esperance (Tunisia)

Mamelodi Sundowns (South Africa) vs Al Ahly (Egypt)

Horoya (Guinea) vs Wydad Athletic Club (Morocco)

Simba (Tanzania) vs TP Mazembe (DR Congo)

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii