Tetesi za soka Jumamosi 23.03.2019: Sancho, Coutinho, Salah, Dybala, Kroos, Mbappe

Jadon sancho Mchezaji wa England na Borussia Dortmond Haki miliki ya picha EPA
Image caption Manchester United na Paris St-Germain wote wanamuwania Jadon sancho

Manchester United na Paris St-Germain wote wameazimia kuweka dau la kitita cha £70m kwa ajili ya mshambuliaji wa England na Borussia Dortmund Jadon Sancho. (Sun)

Barcelona wako tayari kumuuza Mbrazili forward Philippe Coutinho ikiwa watapokea ofa ya zaidi ya £90m, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26-year atataka kubakia katika La Liga club. (ESPN)

Image caption Mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United Ander Herrera anatumai kukukubali kusaini mkataba mpya na klabu hiyo ingawa Paris St-Germain wanamtaka

Juventus wanajiandaa kumtoa Paulo Dybala kwa £44m ili wamchukue mshambuliaji wa Liverpool mwenye umri wa miaka 26 Mohamed Salah msimu ujao. (Tuttosport via Daily Mail)

Bangi inayovutwa mtaani si salama,wasema watafiti

Je wajua kwamba usingizi huathiri maisha yako?

Unaweza kutimua mbio kiwa na umri wa miaka 80?

Tottenham wako tayari kumtoa mchezaji wa safu ya kulia nyuma Kieran Trippier na Serge Aurier msimu ujao. Everton wameibua tena nia yao kwa mlinzi wa England Trippier, mwenye umri wa miaka 28, ambaye amebakiza miaka miwili ya mkataba wa sasa na kwa anathamani ya takribani £20m. (Sun)

Manchester United inaweza kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya kati wa Real Madrid Toni Kroos kwa £50m msimu ujao. Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 29-alikubali kujiunga na Manchester United kutoka klabu ya Bayern Munich mwaka 2013, lakini badala yake akaenda Madrid mwaka 2014. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kibarua cha Frank Lampard kiko mashakani baada ya mmiliki wa klabu yake kuamua kuiuza

Manchester United wanajiandaa kumshawishi Napoli kwa dau kubwa kwa ajili ya mlinzi Msenegal Kalidou Koulibaly, 27. (Mirror)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United Ander Herrera anatumai kukukubali kusaini mkataba mpya na klabu hiyo licha ya Paris St-Germain kuonyesha nia ya kumtaka . (Daily Telegraph)

Mchezaji huyo mwenye umri wamiaka 29- mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Daily Telegraph)

Manchester United wamegonga mwamba katika mazungumzo yao ya mkataba na mshambuliaji Herrera na Muhispania Juan Mata, mwenye umri wa miaka 30. Wote wanataka kuongezewa pesa ndio waaendelee kubakia Old Trafford, kiwango ambacho United hawako tayari kukitoa. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gunners wameazimia kusaini mkataba na mchezaji safu ya kati wa miaka 22 raia wa Ivory Coast Franck Kessie kutoka AC Milan

Kibarua cha meneja Frank Lampard kiko mashakani kwa siku za usoni kwenye klabu yake baada ya mmiliki wa klabu yake Mel Morris kuazimia kubana matumizi kabla ya kuiuza klabu yake. (Times - subscription required).

Mchezaji wa safu ya ulinzi wa Arsenal Stephan Lichtsteiner anasema kuwa hana uhakika kama atakuwa kwenye klabu hiyo msimu ujao, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 kutoka Uswisi anafanya mazungumzo juu ya mkataba wake mpya . (Sky Sports)

Image caption Mlindalango wa Real Madrid Mbelgiji Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 26, anasema yeye ndie bado anashikilia nafasi ya kwanza duniani

Wakati huo huo Gunners wameazimia kusaini mkataba na mchezaji safu ya kati wa miaka 22 raia wa Ivory Coast Franck Kessie kutoka AC Milan. (Tuttomercato - in Italian)

Mlindalango wa Real Madrid Mbelgiji Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 26, anasema yeye ndie bado anashikilia nafasi ya kwanza duniani na amevishutumu vyombo vya habari vya Uhispania kwa "utaka kumuua". (El Espanol via Goal)

Mkurugenzi wa michezo wa Benfica Rui Costa anaamini itakuwa vigumu kuendelea kuwa na mshambuliaji Mreno Joao Felix katika klabu hiyo. Manchester United, Juventus na Liverpool wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka. (Tuttosport - in Italian)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii