Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 25.03.19: Maguire, Keita, Verane, Barella, Bale, de Ligt

Gareth Bale Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bale ameripotiwa kutokuwa na maisha ya furaha ndani ya klabu yake ya Real Madrid

Gareth Bale atakaribishwa tena kwa bashasha katika klabu ya Tottenham iwapo winga huyo raia wa Wales mwenye miaka 29 ataamua kuondoka katika klabu yake ya sasa Real Madrid na kurejea London, amesema beki wa Spurs Ben Davies. (Goal)

Liverpool wanatazamia kumruhusu kiungo Naby Keita, 24, kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu na watakubali kula hasara katika thamani ya mchezaji huyo raia wa Guinea. (Sun)

Klabu za Manchester United, Arsenal na Tottenham zinamnyemelea beki kinda raia wa Denmark anayechezea klabu ya Sampdoria ya Italia Joachim Andersen, 22. (CalcioMercato)

Liverpool watamkosa beki wa kati raia wa Uholanzi anayecheza katika klabu ya Ajax Matthijs de Ligt wakati huu ambapo rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu yupo safarini kwenda kufanikisha makubaliano ya kumnasa mlinzi huyo mwenye miaka 19. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Matthijs de Ligt (kushoto) sasa anatarajiwa kufikia makubaliano ya kujiunga na Barcelona baada ya kuwaniwa vikali pia na klabu za Juventus, Man City na Liverpool

Arsenal wanapanga kumsajili kiungo wa klabu ya Charlton Athletic Joe Aribo, 22, mwishoni mwa msimu. (Mirror)

Manchester United wametaarifiwa kuwa itawalazimu kuvunja rekodi ya usajili ili kumnasa mlinzi raia wa Uingereza Harry Maguire, 26, anayekipiga katika klabu ya Leicester. (Star)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Harry Maguire

Liverpool wameingia katika kinyang'anyiro cha kumnyemelea beki wa Inter Milan na raia wa Slovakia Milan Skriniar, 24. (TeamTalk)

Juventus wanatarajiwa kumsaka beki wa Real Madrid Mfaransa Raphael Varane , 25, baada ya mlinzi huyo kuiambia klabu yake kuwa anataka kuihama. (Football Italia)

Haki miliki ya picha Victor Carretero
Image caption Verane (kulia) akipambana na Leo Messi kwenye mchezo wa el classico .

Everton na Newcastle ni miongoni mwa klabu za Ligi ya Primia ambazo zinamfuatilia beki wa kushoto wa klabu ya Olympiakos Leonardo Koutris. Leicester na West Ham pia wanamnyemelea Mgiriki huyo mwenye miaka 23. (TeamTalk)

Maskauti wa Arsenal walikuwa uwanjani wakimtathmini kiungo wa klabu ya Cagliari Nicolo Barella, 22, akifunga goli lake la kwanza kwa timu ya taifa ya Italia katika mchezo dhidi ya Ufini. (Metro)

Mada zinazohusiana