Sarri: Wachezaji wa Chelsea wameshindwa kufikiria zaidi

Mkufunzi maurizio sarri wa Chelsea

Mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri alisema kuwa kushindwa kwao 2-0 na klabu ya Everton kuna maana ya kwamba timu yake imefikia kikomo chake na hilo linaweza kuwa kweli kutokana na sababu kadhaa

Raia huyo wa Itali alikuwa akielezea kuhusu tofauti ya mchezo alioshuhudia katika kipindi cha kwanza na kile cha pili ambapo alielezea kuwa mchezo mzuri zaidi alioshuhudia msimu wote na kipindi cha pili ambapo alielezea kuwa timu yake ilikuwa inacheza kana kwamba ilikuwa imefikia kikomo huku wachezaji wakiwa wakishindwa kufikiria zaidi.

Lakini pengine kikomo hicho kinaweza kutokana na ukufunzi wa kocha huyo , ikibainika kuwa haikuwa mara ya kwanza kwa kocha huyo mwenye umri wa iaka 60 kuishutumu timu yake msimu huu.

Na huenda ndio kikomo cha Chelsea kuwania nafasi nne bora hatua itakayomaanisha kwamba watalazimika kushinda kombe la Yuropa ili kufuzu kwa vilabu bingwa Ulaya.

Huku wakikabiliwa na mechi muhimu dhidi ya kikosi cha Marco Silva ambacho kilikuwa hakijashindwa na timu sita bora tangu mwezi Januari 2017, wageni hao walichanganyikiwa katika kipindi cha pili katika uwanja wa Goodison Park.

Chelsea ilipoteza kwa mara ya tano tangu mwaka huu uanze huku ikiwa ni Fulham pekee ilio na rekodi mbaya zaidi ukiwa ni mfano mwengine wa kikosi cha Chelsea ambacho kilishindwa kujibu kinapojipata nyuma kwa magoli.

Kushindwa kwao kunaiwacha klabu hiyo ya Sarri katika nafasi ya sita katika ligi ya Premia, pointi tatu nyuma ya Arsenal walio katika nafasi ya nne na kuzua maswali magumu ya iwapo Sarri ndio meneja atakayewaondoa katika matatizo yao kwa sasa.

Tatizo ni nini?

Baada ya kipindi cha kwanza Eden Hazard aligonga mwamba wa goli huku naye Ross Barkley akitawala safu ya kati licha ya kuzomewa na mashabiki wa Everton, Chelsea ilionyesha mchezo mbaya ambao haukumfurahisha Sarri, ijapokuwa Everton inapaswa kupongezwa kwa mchezo wao mzuri.

Cha kushangaza kuhusu mashabiki wa Chelsea ni kwamba baada ya kuona timu yao ikipoteza mechi moja kati ya tisa katika kipindi cha dakika 90 tangu walipolazwa 6-0 na Manchester City mwezi februari, mchezo wao mbaya umerudi na kuwaathiri na Sarri ameshindwa kubadili hali hiyo.

Ni vigumu kwa wachezaji kuweza kuelezea mabadiliko kwangu alisema mkufunzi huyo wa zamani wa klabu ya Napoli kuhusu tofauti iliokuwepo katika kipindi cha kwanza na kile cha pili.

''Ni vigumu kuelezea tofauti hiyo. Nadhani fikra zao zilifikia kikomo. Kwa sasa hiki ndicho kilele chetu'' .

Iwapo tutaweza kucheza kama tulivyocheza kipindi cha kwanza basi tutakuwa katika nafasi nyengine katika jedwali.

Tuna tatizo hili kwa sababu tulipoteza mechi kama hii dhidi ya Wolvehampton mwezi Disemba , tulipoteza tena kama hivi , kwetu sisi tumefika kikomo.

Je Sarri ndio mkufunzi atakayebadili matokeo hayo duni?

Haki miliki ya picha PA
Image caption Chelsea imefunzwa na zaidi ya wakufunzi 10 tangu Abrahamovich aichukue klabu hiyo

Sarri amekuwa akiwakosoa wachezaji wake msimu huu akimshutumu Hazard licha ya mchezaji hyo kuwa na asilimia 48 ya mabao ya ligi ya Uingereza katika klabu hiyo.

Lakini kocha huyo aliushangaza ulimwengu aliposema kuwa huenda akafutwa kazi .

Lakini anaonekana kwamba huenda akaendelea kuifunza timu hiyo hadi mwisho wa msimu akisaidiwa na msururu mzuri wa matokeo ya kombe la bara Yuropa wakiwa katika nafasi ya robo fainali ambapo iwapo watashinda itawapatia njia ya kufuzu katika kombe la vilabu bingwa msimu ujao.

Katika hali isio ya kawaida , Sarri atatumai kumaliza msimu huu na baadaye aongeze wachezaji wazuri ambao watasaidia katika kuwazuia kushindwa katika mechi ngumu.

Hatahivyo kuna kikwazo kikubwa kwa suluhu kama hiyo kuafikiwa kufuatia hatua ya klabu hiyo kupigwa marufuku kununua wachezaji wapya hadi 2020 uamuzi ambao klabu hiyo inajaribu kukata rufaa.

Hatahivyo atapata huduma za winga Christian Pulisic aliyenunuliwa kwa dau la £58m na wachezaji wengine 40 waliopo katika mkopo.

Hali hiyo inachochewa zaidi na uvumi kwamba huenda Hazard akajiunga na Real Madrid huku winga Callum Hudson Odoi akinyatiwa na Bayern Munich ambaye aliwasilisha ombi la kutaka uhamisho mnamo mwezi Januari kutokana na uhaba wa kushirikishwa katika mechi.

Inawezekana Chelsea kuwa katika nafasi nne bora- Sarri

Kwa sasa matatizo hayo yapo katika siku za usoni na Sarri hajakata tamaa.

Alipoulizwa iwapo ana wasiwasi kuhusu matimaini ya timu yake kuwepo katika nafasi ya timu nne bora , alisema: Iwapo unazungumzia kipindi cha pili uko sawa kabisa Iwapo tutacheza kama vile tulivyocheza katika kipindi cha pili basi tuna tatizo la kuwepo katika nafasi nne bora.

''Tunahitaji kupata pointi tatu pekee ili kuwa miongoni mwa timu nne bora. Nina wasiwasi kuhusu hali yetu ya kifikra lakini iapoi tutacheza dakika 90 katika mechi nane kama vile tulivyocheza katika kipindi cha kwanza chochote kinawezekana''.

Sarri anaweza kufurahishwa na mchezo wa kipindi cha kwanza wa Chelsea ambao ulikuwa mzuri lakini kitu muhimu ni kwamba walishindwa kufunga.

Alipendelea kumuanzisha mchezaji wake mpya Gonzalo Higuain ambaye alipona badala ya Olivier Giroud ambaye alifunga hat-trick katikati ya wiki katika mechi ya Yuropa dhidi ya Dynamo Kiev.

Kinyanganyiro cha ligi ya Uingereza cha timu nne bora
Arsenal Chelsea Man Utd Tottenham
31 Machi: Cardiff (Ugenini) 30 Machi: Watford (Nyumbani) 31 Machi: Liverpool (Ugenini)
1 Aprili: Newcastle (Nyumbani) 2 Aprili: Wolves (Ugenini) 3 Aprili: Crystal Palace
7 Aprili: Everton (Ugenini) 8 Aprili: West Ham (Nyumbani) 7 Aprili: Brighton (Nyumbani)
15 Aprili: Watford (Ugenini) 14 Aprili: Liverpool (Ugenini) 13 Aprili: West Ham (Nyumbani) 13 Aprili: Huddersfield (Nyumbani)
20 Aprili: Crystal Palace (Nyumbani) 22 Aprili: Burnley (Nyumbani) 21 Aprili: Everton (Ugenini) 20 Aprili: Manchester City (Ugenini)
24 Aprili: Man City (Nyumbani)
29 Aprili: Leicester (Ugenini) 28 Aprili: Man Utd (ugenini) 28 Aprili: Chelsea (Nyumbani) 27 Aprili: West Ham (Nyumbani)
4 Mei: Brighton (Nyumbani) 4 Mei: Watford (Nyumbani) 4 Mei: Huddersfield (Ugenini) 4 Mei: Bournemouth (ugenini)
12 Mei: Burnley (ugenini) 12 Mei: Leicester (Ugenini) 12 Mei: Cardiff (Nyumbani) 12 Mei: Everton (Nyumbani)
TBC: Wolves (Ugenini) TBC: Brighton (Nyumbani)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii