Conor McGregor: Aliyekuwa bingwa wa zamani wa UFC amestaafu

Conor McGregor na Floyd Mayweather Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Conor McGregor (kulia amedaiwa kujipatia $30m katika pigano dhidi ya Floyd Mayweather 2017

Bingwa wa mizani miwili katika mchezo wa ngumi, mieleka na mateke UFC Conor McGregor anasema kuwa amestaafu rasmi kutoka katika mchezo huo unaojulikana kama 'Mixed Martial Art'".

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 30 alitangaza uamuzi wake katika mtandao wa kijamii siku ya Jumanne.

"Nawatakia kila la kheri wenzangu katika siku za mbeleni '', aliomngezea.

Pigano la mwisho la McGregor lilikamilika huku bondia huyo akipoteza wakati aliposhindwa na Khabib Nurmagomedov mnamo Oktoba 2018 huku raia huyo wa Urusi akishinda pigano hilo katika raundi ya nne.

Lilikuwa pigano lake la kwanza katika ukumbi huo katika kipindi cha miaka miwili na kushindwa kwake kulitokana na ghasia kabla ya pigano hilo hatua iliopelekea wapiganaji wote wawili kupigwa faini na kusimamishwa .

Jinsi McGregor alivyopanda Ulingo wa UFC

McGregor alishinda taji la uzani wa featherweight baada ya kumpiga kwa njia ya knockout Jose Aldo ndani ya sekunde 13.

Baada ya kushindwa kwake na Nate Diaz katika uzani wa Welterweight na hivyobasi kusitisha msururu wa ushindi wake uliokuwa mapigano 15 raia huyo wa Ireland alishinda marudio miezi mitano baadaye.

Ushindi wake dhidi ya Eddie Alvarez ulimthibitisha MCGregor kuwa bingwa wa mizani miwili.

Na katika kilele cha mchezo wake alikubali kukabiliana na bingwa mara tano katika uzani wa Welterweight Floyda Mayweather katika pambano lililoitwa Money Fight{ pigano la fedha}.

Pigano hilo lilimpatia McGregor takriban $30m na kuvutia wanunuzi milioni moja wa mechi hiyo nchini Uingereza na milioni 4 Marekani huku raia huyo wa Marekani akishinda katika raundi ya 10 kwa njia ya Knockout.

Hatahivyo muda wa McGregor katika mchezo huo pia ulikumbwa na utata.

Mwaka 2018 aliagizwa na mahakama kupewa mafunzo ya kuzuia hasira yake na kuhudumia jamii kwa siku tano kutokana na mashtaka ya uhalifu yaliofutiliwa mbali baada ya kushambulia basi lililokuwa na mpinzani wake wa UFC.

Kanda za video zilionyesha McGregor akilirushia chuma basi lililokuwa likimbeba Khabib na baadhi ya wapiganaji wa UFC .

Mapema mwezi huu McGregor alikamatwa mjini Miami kwa kuvunja simu ya shabiki mmoja wakati walipokuwa wakimpiga picha.

McGregor ambaye amemaliza akiwa na rekodi ya ushindi wa mapigano 21 na kushindwa mara nne alisema: Kwa sasa najiunga na wenzangu wa zamani waliostaafu.

Je ni kweli amestaafu?

Hii sio mara ya kwanza kwamba McGregor ametangaza kustaafu kutoka katika mchezo huo.

Mnamo mwaka 2016 mwezi Aprili, McGregor alituma ujumbe wa twitter: 'Nimeamua kustaafu nikiwa kijana Ahsanteni sana'' , lakini muda mchache baadaye alirudi na kusema kuwa hajastaafu bali alikuwa amekosona na wasimamizi wa ukuzaji wa mapigano yake.

Mnamo mwezi Septemba 2018 McGregor alianzisha pombe ya Whiskey kutoka Ireland.

Na kufuatia matamshi ya McGregor kustaafu rais wa UFC Dana White alisema: Ana fedha za kustaafu.

Tunaelewa ningekuwa mimi ningestaafu. Anastaafu kutoka kupigana sio kufanya kazi. Whiskey yake itamfanya awe na kazi ya kufanya na nina hakika ana mambo mengine ya Kufanya.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii