Callum Hudson-Odoi: Chelsea yatoa ushauri kwa winga baada ya kubaguliwa

Callum Hudson-Odoi Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Callum Hudson-Odoi alichezea Englandmara ya kwanza katika mchezo wao dhidi ya Montenegro Jumatatu

Chelsea imetoa ushauri kwa winga Callum Hudson-Odoi baada ya kukabiliwa na ubaguzi wa rangi mara mbili kwa kipinchi cha siku 11

klabu hiyo iliripoti kuwa Callam mwenye umri wa miaka 18 alisikia sauti za mashabiki zikisema nyani wakati wa ushindi wa Chelsea wa kombe la Ulaya Dynamo Kiev tarehe 14 Machi jambo ambalo Uefa wanalifanyia uchunguzi.

Hudson-Odoi alikuw ammoja wa wachezaji wa England waliotukanwa walipopata ushindi wa 5-1 dhidi ya Montenegro Jumatatu.

Meneja wa England Gareth Southgateamekuwa akizungumza na mcheza huyo.

Baada ushindi wa Montenegro ambapo ilikuwa mara ya kwanza kwa Hudson-Odoi kuichezea England, winga huyo alielezea tusi hilo - ambalo pia liwalenga Danny Rose na Raheem Sterling - kama "lisilokubalika ".

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hudson-Odoi alimueleza mchezaji wa Chelsea esar Azpilicueta (kushoto) kuhusu mashabiki waliombagua abaada ya mchezo wa kuwania kombe la Ligi ya Uropa Dynamo Kiev

Nyota huyo mchanga anasemeka anaendelea vizuri tangu wakati huo, lakini atapewa msaada wa aina mbali mbali.

Uefa ilisema "mchakato wa nidhamu " umeanzishwa dhidi ya Montenegro kwa kosa moja la "tabia ya ubaguzi wa rangi".

Hudson-Odoi alisema baada ya kufuzu kwa Euro 2020: "unaposikia mambo kama hayo kutoka kwa mashabiki , sio sawa na haikubaliki . Natumai Uefa italishughulikia ipasavyo.

"Wakati mimi na Rosey tulipokwenda pale, walikuwa wanasema 'ooh aa aa' wakiigiza sauti za nyani - ilibidi tujikaze tu tukaangalia mbele na kujaribu kuwa imara kiakili ."

Meneja wa England Gareth Southgate alisema: "Tunapaswa kuhakikisha wachezaji wetu wahisi wanaungwa mkono , wanajua chumba cha kuvaa jezi kiko pale na kuwa kikundi cha wahudumu wetu kiko pale kwa ajili yao ."

Chelsea watakutana na Cardiff City Jumapili katika mchezo wa marudiano wa Primia Ligi baada ya mapumziko ya michezo ya kimataifa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii