Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 29.03.2018: Pogba, Hudson-Odoi, Jimenez, Koulibaly, Umtiti, Solskjaer

Paul Pogba Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Je Manchester United itamtoa Pogba kwenda Real Madrid mwishoni mwa msimu?

Real Madrid wanapanga kutoa kitita cha pauni milioni 125 ili kumsajili kiungo Paul Pogba,26, kutoka Manchester United. (Sun)

Chelsea wanapanga kumpatia Callum Hudson-Odoi kandarasi mpya ya mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki ili kumshawishi mchezaji huyo kinda mwenye miaka 18 asiondoke klabuni hapo. (London Evening Standard)

Klabu ya Wolves wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa streka Raul Jimenez, 27, kutoka Mexico kwa rekodi ya usajili ya klabu hiyo ya pauni milioni 25. (Telegraph)

Kocha Carlo Ancelotti amesema Napoli hawatalizimika kumuuza beki wao mwenye thamani ya pauni milioni 130 Kalidou Kouliably, 27, ambaye amekuwa akiwindwa na Manchester United kwa muda mrefu. (Mail)

Ole Gunnar Solskjaer amefichua kuwa maajenti wengi wamekuwa wakiwasiliana na Manchester United ili kujaribu kuhamishia wachezaji wao kwenye klabu hiyo mwishoni mwa msimu. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ole Gunnar Solkjaer ameleta matumaini mapya kwenye kikosi cha Manchester United toka alipochukua usukani mwezi Disemba

Ila wachezaji Jadon Sancho, 19, wa Borussia Dortmund na beki wa Real Madrid's Rafael Varane, 25, ndiyo wanaopigiwa upatu zaidi kujiunga na Manchester United katika msimu ujao wa usajili. (Independent)

Miamba ya Ujerumani klabu ya Bayern Munich wanapanga kuvunja rekodi yao ya usajili kwa kuwekeza pesa nyingi zaidi katika dirisha la usajili la mwisho wa msimu huu. (Marca)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Samuel Umtiti akiwa natimu yake ya taifa ya Ufaransa

Arsenal wanaripotiwa kufanya mazungumzo na Barcelona ili kumsajili beki wao Samuel Umtiti, 25. (Gazetta dello Sport, via Mirror)

Kocha mpya wa Leicester City Brendan Rodgers amesema klabu hiyo itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa wachezaji wao nyota watasalia klabuni hapo mwishoni mwa msimu. (Leicester Mercury)

Mada zinazohusiana