Paul Pogba: Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane anampenda mshambuliaji wa Man Utd 'sana'

Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba na meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane Haki miliki ya picha Getty Images & EPA
Image caption Paul Pogba (kushoto)alisaidia Ufaransa kushinda Kombe la Dunia la mwaka 2018 nchini Urusi

Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema mchezaji wa Manchester United Paul Pogba, ambaye amekuwa akisemekana kuhamia Bernabeu, "anajua kufanya kila kitu uwanjani ".

Pogba, mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akisemekana kuwa anataka kuhamia katika klabu ya Bernabeu ya Uhispania na aliwashahi kuielezea Real kama ''timu ya ndoto yake'' alipokuwa akichezea timu ya taifa ya Ufaransa.

"Ninamfahamu binafsi " alisema nahodha wa zamani wa Ufaransa Zidane kabla ya mechi baina ya Real Madrid na Huesca Jumapili.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Paul Pogba alishinda magoli tisa tangu Ole Gunnar Solskjaeralipochukua nafasi ya Jose Mourinho kama meneja mwezi Disemba

"Anamchango mkubwa sana uwanjani na ni wachezaji wachache wanaoweza kukifanya anachokifanya yeye uwanjani ."

Pogba alijiunga tena na United kutoka Juventus ambapo alivunja rekodi ya dunia ya mchezaji anayelipwa vizuri zaidi kwa kulipwa pauni milioni 89 mwaka 2016, lakini hatma yake katika Old Trafford ilionekana kuwa na utata mapema msimu huu huku kukiwa na taarifa za malumbano baina yake na aliyekuwa kocjha wa klabu hiyo Jose Mourinho.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Pogba ni mchezaji wa safu ya kati ya mashambulizi anayeelewa jinsi ya kuzuwia na namna ya kushambulia, alisema Zidani

Ole Gunnar Solskjaeralichukua nafasi ya Mourinho ambaye alifutwa kazi mwezi Disemba mwaka jana na kiwango cha mchezocha Pogba tangu wakati huo kimepanda , ambapo katika kombe la dunia la 2018 World Cup alifunga mabao tisa dhidi ya Norway.

"Ni mchezaji wa safu ya kati ya mashambulizi anayeelewa jinsi ya kuzuwia na namna ya kushambulia," aliongeza Zidane, ambaye alirejea real Madrid tarehe 11 Machi miezi 10 baada ya kuondoka Bernabeu.

"lakini sio mchezaji wangu, yuko Manchester.

"Amekuwa akisema hivyo mara kwa mara, baada ya Manchester, Madrid imekuwa ikimtaka . Kwa hiyo akimaliza muda wake Manchester, kwanini asije hapa Madrid?"

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii