Mkusanyiko wa habari za kandanda Alhamisi: Man United huenda ikawaachilia wachezaji sita mwisho wa msimu kuondoka

Wachezaji sita huenda wakaondoka Old Trafford mwisho wa msimu huu Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Juan Mata - aliyesainiwa kwa dau la £37.1m kutoka Chelsea mnamo mwezi januari 2014 - hana kandarasi mpya mwezi Juni

Manchester United huenda ikawaachilia wachezaji sita kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu wakati timu hiyo ikijiandaa kumuunga mkono mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer katika soko la uhamisho.

Hatahivyo mipango yao inakanganya kuhusu hatma ya kiungo wa kati Ander Herrera, Juan Mata na Alexis Sanchez.

Solskjaer ataamua iwapo Sanchez ataondoka lakini mshahara wa mshambuliaji huyo huenda ukawazuia wanaomuhitaji.

United inawasiliana na Herrera na Mata ambao kandarasi zao zinakamilika msimu huu.

Hatahivyo hakuna utata wa iwapo makubaliano yataafikiwa na wachezaji wote wawili.

Chanzo kimoja kimeambia BBC kwamba Herrera tayari amekubali kujiunga na PSG msimu ujao, ijapokuwa hilo halijathibitishwa na wawakilishi wake ama klabu hiyo.

Sanchez alianzishwa mechi tano pekee huku akicheza kama mchezaji wa ziada mara sita na kufunga goli moja tangu Solskjaer kumrithi Jose Mourinho tarehe 19 Disemba.

Tottenham yavunja rekodi ya dunia kwa kupata faida ya £113m

Tottenham Hotspur ilijipatia rekodi iliovunja rekodi ya dunia ya £113m baada ya kodi msimu uliopita.

Fedha hizo zimeshinda faida ya £106m ilizopata Liverpool mapema mwaka huu.

Matokeo ya kila mwaka ya kifedha ya msimu 2017-18 yanaonyesha kwamba mapato ya Spurs yalipanda kutoka £310m hadi £380m kutokana na mauzo ya wachezaji, mashabiki wengi waliojitokeza katika uwanja wa Wembley na kufuzu katika awamu ya muondoano ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.

Takwimu hizo zilitolewa wakati ambapo klabu hiyo ilikuwa ikifungua uwanja wake mpya wa £1bn huku gharama hiyo ikiwa iliafikiwa kupitia mikopo.

Mapato yake katika ligi ya EPL yaliongezeka maradufu kutoka £19m hadi £42.6m kufuatia ongezeko la mshabiki katika uwanja wa Wembley.

Tottenham iliishinda Crystal Palace 2-0 katika uwanja wao mpya.

Zinedine Zidane apata kichapo cha kwanza

Haki miliki ya picha Getty Images

Real Madrid ilifungwa kwa mara ya tisa katika mechi ya ligi ya La Liga msimu huu huku ikiwa wamepoteza kwa mara ya kwanza tangu ujio wa kocha mpya Zinedine Zidane dhidi ya Valencia.

Kufuatia matokeo hayo, klabu hiyo imepoteza mechi nyingi zaidi ya misimu yao mwili iliopita ikijumlishwa.

Concalo Guedes aliwafungia wenyeji katika kipindi cha kwanza huku Ezequiel Garay akifunga kupitia kichwa.

Karim Benzema alifunga goli la kufutia machozi katika dakika za lala salama lakini hakukuwa na muda zaidi wa kusawazisha.

Haki miliki ya picha Getty Images

Wolves yamsaini mshambuliaji wa Benfica kwa dau la £30m

Wolves wamethibitisha kumsaini mshambuliaji wa Benfica Raul Jimenez kwa dau lililovunja rekodi la £30m.

Raia huyo wa Mexican, 27, amefunga magoli 15 katika mechi 37 tangu alipojiunga na klabu hiyo mwezi Juni 2018.

Ameisaidia Wolves kufika katika nafasi ya saba katika jedwali la ligi na alikuwa kiungo muhimu katika ushindi wa nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Watford.

PSG yafuzu fainali dhidi ya Rennes

Haki miliki ya picha Getty Images

Paris St-Germain ilitinga fainali ya kombe la Ufaransa dhidi ya Rennes baada ya kuilaza klabu ya Nantes katika nusu fainali

PSG imeshinda taji hilo mara 12 na inatarajiwa kuwika kwa mara ya tano mfululizo katika uwanja wa Stade de France siku ya Jumamosi , Aprili 27

Marco Verratti alifunga mkwaju wa chini chini huku naye , Kylian Mbappe akiongeza bao la pili kupitia mkwaju wa penalti - baada ya kushindwa kucheka na wavu hapo awali kabla ya Dani Alves kuongeza bao la tatu.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii