Kwa nini Lionel Messi ndio changamoto inayomkumba Pep Guardiola na Man City

Messi na Pep Guardiola

Barcelona na Lionel Messi ndio sababu kuu ambayo nadhani Manchester City haitaweza kushinda makombe manne msimu huu.

Nikitazama droo ya vilabu bingw Ulaya, iwapo kikosi cha Pep Guardiola kitatinga fainali basi nitataraji kwamba Barcelona watakuwa wapinzani wao mjini Madrid na sidhani kwamba watawashinda.'

Itakuwa mechi nzuri ;lakini timu yoyote ambayo Messi atakuwa akiichezea ndio itakayopigiwa upatu. City kwanza wana changomoto ya kutinga fainali hiyo kwanza.

Hawajakutana na timu kali Ulaya kufikia sasa na hapo ndiposa watakutana na wapinzani wao wakuu msimu huu.

Haki miliki ya picha Alamy
Image caption Kufikia sasa City imezishinda Hoffenheim, Shakhtar Donetsk, Lyon na Schalke ili kutinga robo fainali

Watalazimika kuilaza Tottenham katika robo fainali , ijapokuwa awamu ya kwanza ya robo fainali siku ya Jumanne katika uwanja mpya wa Spurs itakuwa mechi nzuri kwao.

Iwapo watapita watakutana na Juventus ama Ajax katika nusu fainali .

Bado haitakuwa rahisi kwa kuwa mechi hiyo huenda ikawa kali zaidi.

Naamini kwamba wataweza kushinda mataji mengine matatu, lakini kombe la vilabu bingwa itakuwa vigumu.

'Taji la ligi ya Uingereza litakuwa na ushindani mkali hadi mwisho'.

Huku wakiwa na mechi 12 zilizosalia , City inaweza kutazama mechi walizosalia nazo na kujua kwamba wanakaribia kushinda mataji kadhaa.

City tayari imetia kibindoni kombe la Ligi na nadhani pia wataweza kushinda kombe la FA.

Watford waliwasumbua sana katika uwanja wa Etihad mwezi Machi na City walifanikiwa kuongoza kupitia bao la utata la Raheem Sterling ambalo lilidaiwa kuwa la kuotea kabla ya kuhalalishwa.

Kucheza dhidi yao siku ya fainali haitakuwa rahisi , lakini ni mechi ambayo ujuzi wao utawasaidia kushinda.

Ligi ya Premia ni ngumu sana, lakini iko mikononi mwao, iwapo Guardiola atashinda mechi zake zote sita basi watakuwa mabingwa.

Sidhani kwamba watashinda mechi zote sita , lakini tunazungumzia kuhusu timu ambayo imeshinda mechi 22 kati ya 23 katika mashindano yote hivyobasi haitanishangaza iwapo wataibuka mshindi.

Hatahivyo kuna mechi za hila dhidi ya City , wakianza Crystal Palace wikendi ijayo.

Makombe manne yanayonyatiwa na City
Tarehe Wapinzani Tarehe Wapinzani
9 Aprili Tottenham (Ugenini)* 30 Aprili/1 Mei Vilabu bingwa nusu fainali (Nyumbani)
14 Aprili Crystal Palace (Ugenini) 4 Mei Leicester (Nyumbani)
17 Aprili Tottenham (Nyubani)* 7/8 Mei Vilabu Bingwa nusu fainali(Ugenini)
20 Aprili Tottenham (Nyumbani) 12 Mei Brighton (Ugenini)
24 Aprili Man Utd (Ugenini) 18 Mei FA Cup final (Neutral)
28 Aprili Burnley (Ugenini) 1 Juni CL final (Neutral)

Palace tayari wameishinda City msimu huu kabla ya krisimasi wakati Andros Townsend alipofunga goli katika uwanja wa Etihad huku The Eagles pia wakikosa Penalti dhidi yao msimu uliopita ambayo ingesitisha msururu wa matukio mazuri ya City.

Kikosi cha Roy Hodgson kimefanya vizuri ugenini zaidi ya nyumbani katika uwanja wa Selhurst Park msimu huu lakini watakuwa wapinzani hatari.

Mechi ngumu ambayo ipo mbele yao ni ile ziara ya uwanja wa Old Trafford baadaye mwezi Aprili lakini picha hapo juu huenda ikawa imebadiliko kufikia wakati huo.

Sidhani kwamba Liverpool itashinda kila mechi , na United ugenini haitakuwa mechi ambayo City lazima ishinde ili kuendeleza nafasi yao ya kushinda ligi.

Kukosekana kwa Aguero ni pigo kurudi kwa De Bruyne ni jeki

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Aguero (kushoto] ndio mfungaji wa magoli mengi katika ligi ya EPL

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii