Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 13.04.2019: Pogba, Eriksen, Kroos, De Ligt, Mane, Wan-Bissaka

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema kuwa kichwa cha Paul Pogba hakitageuzwa na Real Madrid Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema kuwa kichwa cha Paul Pogba hakitageuzwa na Real Madrid

Real Madrid itaangalia uwezekano wa kumtoa kiungo wa kati mjerumani Toni Kroos mwenye umnri wa miaka 29 msimu ujao ili kupata nafasi ya kumuajiri Mfaransa Paul Pogba anayechezea Manchester United kwa sasa akiwa na umri wa miaka , 26, na mchezaji wa Tottenham Christian Eriksen raia wa Denmark. (AS)

Hata hivyo wameanza mazungumzo ya awali kwa ajili ya kusaini mkataba na Eriksen mwenye umri wa miaka 27 na mkataba huo unaweza kugharimu zaidi ya Euro milioni 100. (Tuttosport, via Calciomercato)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Manchester United wamesema hawana nia tena ya kumchukua mchezaji wa Crystal Palace Muingereza Wan-Bissaka

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema kuwa kichwa cha Paul Pogba hakitageuzwa na Real Madrid, licha ya kumshawishi kwa mkataba unaoandaliwa kwa ajili yake wa £130m . (Mirror)

Meneja wa Everton Marco Silva anasema kuwa "ameshangazwa " na taarufa za uvumi kwamba winga wao Theo Walcott mwenye umri wa miaka 30 anahama kutoka Goodison. (Liverpool Echo)

Manchester United wamesema hawana nia tena ya kumchukua mchezaji wa Crystal Palace Muingereza Wan-Bissaka mwenye umri wa miaka 21, huku wakisema wanapendelea zaidi kumchukua mlinzi wa Paris St-Germain na tiumu ya Ubelgiji Thomas Meunier, mwenye umri wa miaka 27. (sun)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Everton wasema kamwe winga wao Theo Walcott mwenye umri wa miaka 30 hatahama Goodison

Mshambuliaji wa Everton Oumar Niasse yuko tayari kufanya mazungumzo na meneja wa Silva baada ya kuhamia Cardiff mwezi Januari . (Star)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Meneja wa zamani wa Manchester United Louis Van Gaal amemshauri Mchezaji wa timu ya Uholanzi Matthijs de Ligt ajiunge na Manchester City au Barcelona

Mchezaji wa safu ya kati -nyuma wa timu ya Uholanzi Matthijs de Ligt, mwenye umri w amiaka 19, ataondoka Ajax akiamia Bayern Munich au Barcelona msimu ujao, kwa mujibu wa meneja wa timu ya taifa ya Ujerumani Erik ten Hag. (Suddeutsche Zeitung - in Dutch)

Na badala yake , mchezaji mwenza De Ligt na meneja wa zamani wa Manchester United Louis Van Gaal anasema mlinzi huyo anapaswa kujiunga na Manchester City au Barcelona msimu huu , kuliko kuhamia Juventus. (Gazzetta - in Italian)

Real Madrid bado ina hamu kubwa ya kumchukua mchezaji wa Liverpool Msenegali anayecheza katika safu ya mashambulizi Sadio Mane, lakini timu hiyo kubwa katika ligi ya Uhispania itachukua hatua hiyo iwapo tu kijana huyo mwenye umri wa miaka 27-year-atawadsiliusha maombi ya kuhama. (El Confidencial - in Spanish)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Real Madrid bado ina ya kumchukua mshambuliaji wa kati wa Liverpool Sadio Mane

Bournemouth wanaangalia kama wanaweza kumnunua winga wa Uskochi Ryan Fraser mwenye umri wa miaka 25 huku winga huyo akisakwa pia Arsenal. (Mirror)

Wakati huo huo mshambuliaji wa kati wa Cherries Callum Wilson, ambaye ilisemekana anahamia Chelsea Chelsea mwezi Januari anasema anafurahia kuichezea Eddie Howe na hataki kujipata akicheza katika klabu ya Bournemouth. (Star)

Tottenham wamejipanga kulipa £30m ili kusaini mkataba na rais wa Ureno anayeichezea Barcelona safu ya kati Andre Gomes baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kukamilisha deni lake katika Everton. (Star)

Manchester United wamemlipa mshahara karibu mara dufu Ander Herrera Muhispani mwenye umri wa miaka 29 ili aendelee kubakia kwenye klabu hiyo. (Forbes)

Mchezaji wa safu ya nyuma kulia wa Paris St-Germian Dani Alves, mwenye umri wa miaka 35,amewakosoa wazi wachezaji wenzake katika timu hiyo katika mahojiano na redio ya Ufaransa. Mbrazil huyo alidai klabu hiyo ingepaswa kuwa imezingati ushauri wake kwasababu ya uzoefu wake katika viwango vya juu vya soka (RMC radio, via AS)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii